Showing posts with label Lady Jay Dee. Show all posts
Showing posts with label Lady Jay Dee. Show all posts

Monday, 3 October 2016

SAWA NA WAO LYRICS BY LADY JAYDEE



LYRICS

   Sawa Na Wao’ is all about life, love, relationships and portraits life through the lens of a relationship and some of those temptations distractions that often disrupts or destroy those relationships. Lady Jaydee's next smash hit release through her worldwide exclusive partnerships with her record label and management company ROCKSTAR4000, publishing partnership with 'Rockstar Publishing' and Content Partnership with RockstarTV.

The ‘Sawa Na Wao’ music video was Directed by the phenomenal Director Meji.

Fans can follow Lady Jaydee on any of her official social media and digital networks:

Lyrics will be available soon

Friday, 22 July 2016

WANAUME KAMA MABINTI LYRICS BY LADY JAY DEE FT PAPII KOCHA

[Chorus – Lady Jay Dee]
Mnakula, kunywa na kuvaa siku zinaenda
Vya bure hupenda kupewa, wala hamna fikira
Kila upande mna-fit, siku zinaenda
Vinywa vimejaa ufitini, wanaume kama mabinti
[Verse 1 – Lady Jay Dee]
Hivi nini kimewauma? Sikumaanisha wote
Na kama kweli hakikuhusu, hakiwezi kuuma
Najua wazi mnaelewa, ila mu wabishi
Hamtaki kukubali huu ukweli halisi
Vyovyote itavyokuwa ujumbe wangu mmeupata
Hata mkijifanya hamtaki vyema kuelewa
Fanyeni kazi vijana ili tuijenge nchi
Kamwe msikubali kufananishwa na machangudoa
[Chorus – Lady Jay Dee]
Mnakula, kunywa na kuvaa siku zinaenda
Vya bure hupenda kupewa, wala hamna fikira
Kila upande mna-fit, siku zinaenda
Vinywa vimejaa ufitini, wanaume kama mabinti
[Verse 2 – Papii Kocha]
Ebwana sema, sema, sema, haki yako Jay Dee
Tembo kuvaa vipusa halali haki yako Zey D
Inakuwa vipi wanaume muwe tegemezi?
Japokuwa kweli wamama wanawapeni mapenzi
Mkivishwa magauni na vimini mtachukia
Acheni basi kama hamtaki, ya kuambiwa ukweli ukweli
[Chorus – Lady Jay Dee]
Mnakula, kunywa na kuvaa siku zinaenda
Vya bure hupenda kupewa, wala hamna fikira
Kila upande mna-fit, siku zinaenda
Vinywa vimejaa ufitini, wanaume kama mabinti
[Verse 3 – Lady Jay Dee]
Ukiwakuta kwenye vikao, oh vya pombe
Eti wao wasemaji, wanaojua yote
Hawatoi hata senti ya kulipa bili
Ikifika zamu yao huenda msalani
Kwa ukuwadi namba moja wao hupenda
Wanaopenda kuwaliwaza mademu wa wenzao
Shoga zangu hebu leteni magauni tuwavishe
Hijabu tuwafunge, na vimini, vitopu tuwaazime
[Chorus – Lady Jay Dee]
Mnakula, kunywa na kuvaa siku zinaenda
Vya bure hupenda kupewa, wala hamna fikira
Kila upande mna-fit, siku zinaenda
Vinywa vimejaa ufitini, wanaume kama mabinti
[Bridge]
[Lady Jay Dee]
Papii umeona wapi mwanaume kunyweshwa pombe?
[Papii Kocha]
Jay Dee hivi tangu lini, rijali zima likasutwa?!
[Lady Jay Dee & Papii Kocha]
Nilishangaa ya jana, ati nae kaja kitchen party, olala
[Chorus – Lady Jay Dee] x2
Mnakula, kunywa na kuvaa siku zinaenda
Vya bure hupenda kupewa, wala hamna fikira
Kila upande mna-fit, siku zinaenda
Vinywa vimejaa ufitini, wanaume kama mabinti
[Outro – Papii Kocha & (Lady Jay Dee)]
Igwe, igwe lele lele (igwe lele lele)
Igwe, igwe lele lele, ah, ah, igwe lele lele
Igwe lele lele, ah, ah, igwe lele lele
Lele lele (lele lele) ah, ah, igwe lele lele
(Igwe lele lele)
Igwe, igwe lele lele (igwe lele lele)
Igwe yoyo, igwe lele lele
Igwe, igwe lele lele (igwe lele lele)
Ah, ah, ah, ah, igwe lele lele
Lady Jay Dee, uko Papii Kocha eeh
(Mika Mwamba, na Norman Dikaka)

PUMZIKO LYRICS BY LADY JAY DEE

[Chorus]
Mwambie wataka kuja
Huru apate kuachia
Maamuzi yako upange
Bila kuwa wake upande
Huoni we wateseka?
Kwake u kama mateka
Wahitaji pumziko
Nipo kwa ajili yako
Njoo nikupe fundisho
Achana na vyake vituko
Nipo kwa ajili yako
Njoo upate pumziko
[Verse 1]
Umkalishe kitako
Sema nae taratibu
Hii nafasi ni yako
Usijitie aibu
Kwani na mimi mwenzako
Nasubiri kukutibu
Sitochoka kusubiri
Hadi unipe majibu
[Chorus]
Mwambie wataka kuja
Huru apate kuachia
Maamuzi yako upange
Bila kuwa wake upande
Huoni we wateseka?
Kwake u kama mateka
Wahitaji pumziko
Nipo kwa ajili yako
Njoo nikupe fundisho
Achana na vyake vituko
Nipo kwa ajili yako
Njoo upate pumziko
[Verse 2]
Hana mapenzi juu yako
Kwako yeye miyeyusho
Wahitaji suluhisho
Achana na vituko
Nini anataka kwako?
Muulize akueleze
Sitochoka kusubiri
Hadi unipe-unipe-unipe majibu
[Chorus]
Mwambie wataka kuja
Huru apate kuachia
Maamuzi yako upange
Bila kuwa wake upande
Huoni we wateseka?
Kwake u kama mateka
Wahitaji pumziko
Nipo kwa ajili yako
Njoo nikupe fundisho
Achana na vyake vituko
Nipo kwa ajili yako
Njoo upate pumziko
Mmh, aah, ah ah
Mmh, aah
[Chorus]
Mwambie wataka kuja (uh mwambie)
Huru apate kuachia
Maamuzi yako upange
Bila kuwa wake upande (bila kuwa wake upande)
Huoni we wateseka? (wa… teseka)
Kwake u kama mateka
Wahitaji pumziko
Nipo kwa ajili yako
Mwambie wataka kuja

MUHOGO WA JANG'OMBE LYRICS BY LADY JAY DEE


[Chorus]
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
[Verse 1]
Hadi tamati naapa muhogo sitonunua
Haikuwa Maimuna aliyekwenda ung’oa
Hadi tamati naapa muhogo sitonunua
Haikuwa Maimuna aliyekwenda ung’oa
Kapata tetekuwanga na ugonjwa wa surua
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
[Chorus]
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
[Verse 2]
Kula dori kula dori mshindo wa sufuria
Guriri guriri kofia inavuliwa
Kula dori kula dori mshindo wa sufuria
Guriri guriri kofia inavuliwa
Ndie mimi ndie mimi afatae ukoa
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
[Chorus]
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
[Verse 3]
Mtu akitaka kupa, hakuletei barua
Hukupa usingizini pasi mwenyewe kujua
Mtu akitaka kupa, hakuletei barua
Hukupa usingizini pasi mwenyewe kujua
Kwenda mbio si kupata, bure unajisumbua
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
[Chorus]
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
[Verse 4]
Mkato wake matege wakati anapokuja
Aliiweka dhamiri ya kumvulia koda
Mkato wake matege wakati anapokuja
Aliiweka dhamiri ya kumvulia koda
Wallahi nimeghairi, kiumbe hana mmoja
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
[Chorus]
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
[Verse 5]
Kamfunge kamfunge beberu wa Athumani
Umfunge umfunge pahala panapo jani
Kamfunge kamfunge beberu wa Athumani
Umfunge umfunge pahala panapo jani
Endaeke sina hofu, atarejea ngamani
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
[Chorus]
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
[Verse 6]
Sina ngoa sina ngoa, kuwa daiwa sitaki
Ni mwerevu ni mwerevu, wallahi sihadahiki
Sina ngoa sina ngoa, kuwa daiwa sitaki
Ni mwerevu ni mwerevu, wallahi sihadahiki
Pambanua pambanua, viwili havipendeki
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
[Chorus] x2
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
Muhogo wa Jang’ombe, sijaulamba mwiko
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo

MACHOZI YA FURAHA LYRICS BY LADY JAY DEE


[Verse 1]
Nakupenda mpenzi wa maisha, maisha, maisha
Na mimi moyoni, nafuraha tele moyoni
Kuwa wako mwenzi wa maisha
Katu hayatoisha, toka moyoni mwangu
Nimekuchagua we uwe wangu
Vipingamizi vingi waliweka
Asante Mola tumevuka
Tupamoja sasa, wenye kusema wacha waseme
Nakupenda, wanipenda
Furaha twaidumisha
Nitakuwa wako maisha, utakuwa wangu kabisa
[Verse 2]
Siku yangu imefika, imefika ah aah
Na mimi moyoni, nafuraha tele moyoni
Kukupata mwenzi wa maisha
Nami naahidi nitakupa vyote
Tangu sasa hata milele
Siku yangu imefika, imefika ah aah
Na mimi moyoni, nafuraha tele moyoni
Furaha, furaha, furaha tele moyoni
Furaha, furaha, furaha tele moyoni
[Bridge]
Ee hee, olala lala lala lalalaa
Oo hoo, ooh uuiih
Uuh huu, ulala lala lala
Aa haa, uuh huu
Aa haa, uuh huu
Wawa wawawa
[Verse 3]
Natoa machozi ya furaha, furaha, furaha
Kwani penzi letu limekwishaota mizizi
Umekuwa wangu laazizi
Nami naamini tutaishi sote
Tutapita na pande zote
Nimekuwa wako mahabuba
Kaeni kando, acheni pupa
Tutapita kote, pande zote, mahali pote
Wenye kusema na waseme
Nakupenda, wanipenda
Umekuwa wangu wa maisha, wa maisha ah maisha
Mmh!
[Outro]
Ee hee, ee hee
Ulala lala lala lalala
Ninalo penzi, la milele
Moyoni mwangu
Ninatoa machozi ya furaha ah aa haa
Yee eh, nina furaha
Ninalo penzi, la milele
Ee hee, aa haa
Mmhh!

MWAMBIE UKWELI LYRICS BY LADY JAY DEE

[Intro]
Uh sema nae ah aah
Ukae nae mmh mmh
Uh sema nae ah aah
Utete nae mmh mhh
[Verse 1]
Unacho kitu hautaki kusema
Kwa kuogopa kumuumiza
Leo unaficha, kesho atatoka
Atakutana nayo
Ee mzazi fungua macho
Na ufungue moyo
Umwambie eeh, uokoe maisha yake
[Chorus]
Nachotaka mwambie ukweli wala usimfiche
Kwa manufaa yake, utaokoa maisha yake
Nachotaka mwambie ukweli wala usimfiche
Kwa manufaa yake, utaokoa maisha yake
[Verse 2]
Oh zingatia hali halisi, umwambie ukweli
Jukumu lako kama mzazi, sema nae waziwazi
Vishawishi vipo vingi
Hebu mjengee msingi
Umwambie eh eh, uokoe maisha yake
[Chorus]
Nachotaka mwambie ukweli wala usimfiche
Kwa manufaa yake, utaokoa maisha yake
Nachotaka mwambie ukweli wala usimfiche
Kwa manufaa yake, utaokoa maisha yake
[Bridge]
Uh sema nae ah aah
Ukae nae mmh mmh
Uh sema nae ah aah
Utete nae mmh mhh
Sema nae (uh sema nae)
Ongea nae (ah aah)
Kaa nae (ukae nae)
Umweelezee akuelewe (mhh mmh)
Sema nae (uh sema nae)
Ongea nae (ah aah)
Teta nae (utete nae)
Kwa sauti ya upole (mmh mhh)
[Chorus]
Nachotaka mwambie ukweli wala usimfiche
Kwa manufaa yake, utaokoa maisha yake
Nachotaka mwambie ukweli wala usimfiche
Kwa manufaa yake, utaokoa maisha yake
Uh mwambie…

PENZI LA MILELE LYRICS BY LADY JAY DEE


[Verse 1]
Nilipokuona kaka moyo ulitikisika
Nilipowaelezea katu sikusadikika
Mbele ya Mungu kaka, daima nitakukumbuka
Kwa pendo lako la dhati, pendo lenye uhakika
[Chorus 1]
Nitakuwa nawe mpenzi
Siku zote maishani
Kwani hili lako penzi
Sijaona asilani
Usikonde, usihofu
Kwengine simtumaini
Na kamwe sitakubali
We uende mbali nami
[Verse 2]
Si masihara, si utani
Kama walivyodhani
Na sasa watahamaki
Niko nawe maishani
Naapa ulimwenguni
Sitakuacha asilani
Hawatapata majibu
Ninakupenda kwanini
[Chorus 2]
Nitakuwa nawe mpenzi
Siku zote na milele
Kwani hili lako penzi
Nitalienzi milele
Sitaki mwingine mwenzi
Wala mpiga misele
Na kamwe sitokubali
We uende mbali nami
[Verse 3]
Sioni wa kulivunja, na katu sitomuona
Watabaki kujigonga, lako hawataliona
Mashariki, magharibi penzi lako limwanana
Nikiugua mpenzi, kwa penzi lako ninapona
[Outro]
Hata wakisema sana (waache waseme)
Sitoacha kukuwaza (uh sitowacha)
Kwa kuwa tunapendana (mimi na wewe)
Muda hatutapoteza (ooh)
Yote ni yangu maisha (yangu maisha)
Hakuna wa kujihusisha (nani wa kujihusisha?)
Sitokuacha asilani
Kwako mimi nimekwisha (mmh tarara aah)

RAFIKI MASHAKA LYRICS BY LADY JAY DEE


[Chorus]
Anachonganisha (rafiki)
Anavunja nyumba (rafiki)
Kwa ulimi wake (rafiki)
Huyu rafiki wa mashaka
Kanichonganisha (rafiki)
Kanipakazia (rafiki)
Kanipaka tope (rafiki)
Kila nipitapo mimi sifai
[Verse 1]
Siri zote ametoa yeye
Ya uongo amesema yeye
Kupakaza mi sina kitu
Huyu rafiki wa mashaka
Oh oh najuta (najuta)
Amenisaliti, kwanini? Kwanini?
Nilidhani rafiki oh
[Chorus]
Anachonganisha (rafiki)
Anavunja nyumba (rafiki)
Kwa ulimi wake (rafiki)
Huyu rafiki wa mashaka
Kanichonganisha (rafiki)
Kanipakazia (rafiki)
Kanipaka tope (rafiki)
Kila nipitapo mimi sifai
[Verse 2]
Nikisema sina rafiki, walimwengu niaafikini
Marafiki sio rafiki, wamejawa unafiki
Unampa unalojua ukidhani atalitunza
Dakika chache tu kupita, kona zote kashafikisha
Rafiki upatwapo shida, atakuwepo kushika bega
Na akitoka kukupooza, ukigeuka anakucheka
Kesho kutwa ukipata pesa, wa kwanza kuyapeleka
Kwa kusema eti umekopa, huna uwezo wa kifedha
Rafiki
[Chorus]
Anachonganisha (rafiki)
Anavunja nyumba (rafiki)
Kwa ulimi wake (rafiki)
Huyu rafiki wa mashaka
Kanichonganisha (rafiki)
Kanipakazia (rafiki)
Kanipaka tope (rafiki)
Kila nipitapo mimi sifai
[Verse 3]
Oh nashangaa, bado nashangaa
Huyu rafiki, rafiki gani!
Huyu rafiki, rafiki gani?
Mwenye roho kama gazeti!
Tena gazeti la Ijumaa, lisojua mema ya mtu
Hunisema kwa mabaya tu
Kwani mimi kweli sina jema?
Rafiki huyu hana utu, anachojali ye ni pesa
[Chorus]
Anachonganisha (rafiki)
Anavunja nyumba (rafiki)
Kwa ulimi wake (rafiki)
Huyu rafiki wa mashaka
Kanichonganisha (rafiki)
Kanipakazia (rafiki)
Kanipaka tope (rafiki)
Kila nipitapo mimi sifai
[Outro]
Muongo rafiki huyo, rafiki huyo
Wa mashaka rafiki huyo, rafiki huyo
Mchonganishi rafiki huyo, rafiki huyo
Ameniponza rafiki huyo, rafiki huyo
Mnafiki rafiki huyo, rafiki huyo
Kaa mbali nae rafiki huyo, rafiki huyo
Leo kwangu rafiki huyo, rafiki huyo
Kesho kwa Monica rafiki huyo, rafiki huyo
Ye ni mdaku rafiki huyo, rafiki huyo
Mara kwa Sinta rafiki huyo, rafiki huyo
Nasema ni muongo rafiki huyo, rafiki huyo
Mara vingine kwa Chifupa rafiki huyo, rafiki huyo

MAWAZO LYRICS BY LADY JAY DEE FT AY

[Chorus – Lady Jay Dee]
Mawazo kila mtu anayo mawazo
Tukikaa tukitembea tuna mawazo
Tukilala tukiamka tuna mawazo
Mawazo, mawazo
Haijalishi ni mazuri au mabaya
Suala bado liko pale pale ni mawazo
Tukitembea na tukikaa tunawaza
Mawazo, mawazo
[Verse 1 – Lady Jay Dee]
Hata ukiwa na pesa lazima uwaze
Utapanga bajeti ni nini ukafanye
Ukiwa hunazo pesa ndio yazidi
Utawaza ni wapi uende ukasake
Toto lako likiwa tukutu utawaza ulichape viboko vingapi ili likome
Walimwengu nao wakiwa ni wakusakama
Utawaza ni jinsi gani uwaepuke
Hakuna binadamu asiye na mawazo
Hata vichaa nao huwa wanawaza
Kila kitu duniani lazima uwaze
Hakuna litendekalo bila ya mawazo
[Chorus – Lady Jay Dee]
Mawazo kila mtu anayo mawazo
Tukikaa tukitembea tuna mawazo
Tukilala tukiamka tuna mawazo
Mawazo, mawazo
Haijalishi ni mazuri au mabaya
Suala bado liko pale pale ni mawazo
Tukitembea na tukikaa tunawaza
Mawazo, mawazo
[Verse 2 – Lady Jay Dee]
Hata mimi Jay Dee pia nina mawazo (sexy Lady Jide huuu!)
Wazo langu nataka nunua Freelander
Ila si lazima wazo langu litimie
Wengine wawaza kuiba watajirike
Wengine kuwa warembo wasifike
Mwavita anataka kuwa mwanasheria
Amina kuwa mtangazaji maarufu
Toyoyo kujenga nyumba ya kifahari
Lenee hata yeye kuishi na mzungu
Kila mtu duniani lazima uwaze
Hakuna litendekalo bila ya mawazo
[Chorus – Lady Jay Dee]
Mawazo kila mtu anayo mawazo
Tukikaa tukitembea tuna mawazo
Tukilala tukiamka tuna mawazo
Mawazo, mawazo
Haijalishi ni mazuri au mabaya
Suala bado liko pale pale ni mawazo
Tukitembea na tukikaa tunawaza
Mawazo, mawazo
[Verse 4 – AY]
Mawazo nami, mi na mawazo
Haya ndio maisha yangu ya kila siku wa commercial
Yananitinga mpaka naonekana ka mjinga
Always dili zinakataa lakini haikumkinga
Nikitembea, nikiongea kichwa changu chawaza
Yaani mawazo kibao, yaani ni ya kusaza
Nawazo kuhusu maisha, wapi ntapata pesa
Wapi zipo sasa na ni vipi ntazinasa
Mara nyingine mi nadata
Maisha yamenielemea wengine wananicheka (owh owh owh owh)
Nshasikia wengine washajitoa roho
Machoni naona giza, unafuu hata siuoni
Msaada ntapata wapi kwenye shida hatujuani
Wengine wanaongea peke yao njiani
Yote kuwaza, yote mawazo tu
[Chorus – Lady Jay Dee]
Mawazo kila mtu anayo mawazo
Tukikaa tukitembea tuna mawazo (uuh Jay Dee nina mawazo)
Tukilala tukiamka tuna mawazo
Mawazo, mawazo (kila mtu na mawazo)
Haijalishi ni mazuri au mabaya (uuuh uuh)
Suala bado liko pale pale ni mawazo
Tukitembea na tukikaa tunawaza (uh lala lala lala lalaa)
Mawazo, mawazo

WAWEZA KWENDA LYRICS BY LADY JAY DEE

[Intro]
Oh
Waweza kwenda
Vyovyote utakavyotaka
[Chorus]
Hivi sasa waweza kwenda, waweza kwenda
Kwani sikuhitaji tena maishani mwangu
Uwe wangu, usiwe wangu yote ni sawa
Hivi sasa waweza kwenda, waweza kwenda
Kwani sikuhitaji tena maishani mwangu
Uwe wangu, usiwe wangu yote ni sawa
[Verse 1]
Ulipoondoka nilisikitika
Nilifikiria ni vipi ntakufanya urudi tena
Sitaki majonzi tena, sitaki teseka
Nenda moja kwa moja
Nimekishachoshwa na vyako vingi vioja
Ulisema wanipenda, na mbona ulinitenda!
Wewe hujui kupenda, labda tu wapenda pe-pesa
Na kwa ulivyonitenda, sina budi kukutema
Haya kaka hebu nenda, kha! Kwani nini?!
[Chorus]
Hivi sasa waweza kwenda, waweza kwenda
Kwani sikuhitaji tena maishani mwangu
Uwe wangu, usiwe wangu yote ni sawa
Hivi sasa waweza kwenda, waweza kwenda
Kwani sikuhitaji tena maishani mwangu
Uwe wangu, usiwe wangu yote ni sawa
[Verse 2]
Umerudi tena
Unaniahidi kwamba hutarudia tena
Mbona kabla hujayatenda hukuniahidi?
Kwamba utanilaghai, na kuniona sifai
Si lolote, si chochote
Kwani hata mimi hivi sasa hunifai
Kwanini uliniponza? Baadae ukaniponda
Mfaume wa kupotosha
Ni nini hebu ne-nenda
Sitaki tena kukuwaza, mawazo utanijaza
Sina haja, sina haja, mn-mh, mn-mh!
[Chorus]
Hivi sasa waweza kwenda, waweza kwenda
Kwani sikuhitaji tena maishani mwangu
Uwe wangu, usiwe wangu yote ni sawa
Hivi sasa waweza kwenda, waweza kwenda
Kwani sikuhitaji tena maishani mwangu
Uwe wangu, usiwe wangu yote ni sawa
Hivi sasa waweza kwenda, waweza kwenda
Kwani sikuhitaji tena maishani mwangu
Uwe wangu, usiwe wangu yote ni sawa
[Bridge]
We nenda kaka, ne-nenda
Waweza kwenda
Uh uuh, waweza kwenda
Vyovyote vile utavyotaka
Uh waweza kwenda
[Chorus]
Hivi sasa waweza kwenda, waweza kwenda
Kwani sikuhitaji tena maishani mwangu
Uwe wangu, usiwe wangu yote ni sawa
Hivi sasa waweza kwenda, waweza kwenda
Kwani sikuhitaji tena maishani mwangu
Uwe wangu, usiwe wangu yote ni sawa
Hivi sasa waweza kwenda, waweza kwenda
Kwani sikuhitaji tena maishani mwangu
Uwe wangu, usiwe wangu yote ni sawa
[Outro]
Waweza kwenda
Sikuhitaji
Vyovyote vile utavyotaka
Waweza kwenda…

USIKATAE LYRICS BY LADY JAY DEE FT DULLY SYKES, MR. BLUE, MAD ICE

[Intro]
Maisha kwa wengineo huwa matamu
Lakini kwa wengine huwa magumu
Jiulize ndani ya moyo ni kwanini
Maisha yawe ya utofauti
[Verse 1]
Fungua macho mpe mkono
Fungua moyo toa kidogo
Chochote kile ulicho nacho
Si utajiri bali ni moyo
Aiyo iyo iyo iyo mama iyo
Dunia hii wote tunapita
Nani wa kusema anajivuna
Asiyekufa chini akazikwa?
Labda kesho zamu yako
Mpe leo akupe kesho
Ikifika kesho asipokuwepo
Thawabu peponi yakungoja we
[Chorus]
Usikatae akikuita
Labda kesho yatakukuta
Dunia yabadilika
Hujui lini utaanguka
Usikatae akikuita
Labda kesho yatakukuta
Dunia yabadilika
Hujui lini utaanguka
[Verse 2]
Usikatae akikuita
Labda kesho yanakukuta
Dunia yabadilika wewe
Yabadilika
Kama wote tulizaliwa Afrika, oh ooh
Basi sote ndugu wa mama mmoja
Tusaidiane
Tulipinge balaa hili lilotukuta
Tuokoe ndugu zetu watanzania
Mimi leo naanza kwa kuimba mmh mmh
Baraka ishuke kwetu, balaa liondoke kwetu
Furaha ije tena kwetu, mateso mateso sasa basi!
Itika anapokuita, zaidi ya upoweza
Dunia yabadilika, hujui lini utaanguka
[Chorus] x2
Usikatae akikuita
Labda kesho yatakukuta
Dunia yabadilika
Hujui lini utaanguka
Usikatae akikuita
Labda kesho yatakukuta
Dunia yabadilika
Hujui lini utaanguka
[Bridge]
Usikatae akikuita
Dunia yabadilika
Usikatae akikuita
Dunia yabadilika
Hujui lini utaanguka
[Chorus]
Usikatae akikuita
Labda kesho yatakukuta
Dunia yabadilika
Hujui lini utaanguka
Usikatae akikuita
Labda kesho yatakukuta
Dunia yabadilika
Hujui lini utaanguka

NIMEKUSAMEHE LYRICS BY LADY JAY DEE

[Verse 1]
Nimekusamehe lakini sitokusahau
Visa ulivonitendea Kalala ee, eh
Visa ulivonitendea Jide ee, eh
Ulinikana eh wakati nina shida
Ukasahau yote tuliofanya nawe
Wakati unaelewa hakuna bingwa wa shida
Wakati unaelewa hakuna komando wa shida
Leo nakukumbusha shida huja na kupita
[Pre-Chorus]
Yaliyopita si ndwele tugange yajayo kaka
Kweli nimekusamehe lakini sitokusahau
[Chorus]
Lalalalalalala lalalalala la
Lalalalalalala mimi nimekusamehe
Lalalalalalala lalalalala la
Lalalalalalala mimi nimekusamehe
[Verse 2]
Rafiki wa kweli ni yule asiyekutupa eh
Kwenye dhiki na faraja mko wote, mko wote
Kwenye dhiki na faraja ooh, ooh
Uliniacha nateseka peke yangu, peke yangu
Pasipo msaada wowote kaka oh, oh
Pasipo msaada wowote kaka oh, oh
[Pre-Chorus]
Kweli nimekusamehe lakini sitokusahau
Yaliyopita si ndwele tugange yajayo kaka
[Chorus]
Lalalalalalala lalalalala la
Lalalalalalala mimi nimekusamehe
Lalalalalalala lalalalala la
Lalalalalalala mimi nimekusamehe
[Bridge]
Iyelele mama, iyelele mama, iyelele mama eh
Iyelele mama, iyelele mama, iyelele mama eh
Mamee
Iyelele mama, iyelele mama, iyelele mama Amza Kalala
Iyelele mama, iyelele mama, iyelele mama eh
Mamee
Iyelele mama, iyelele mama, iyelele mama Komando Jide
Iyelele mama, iyelele mama, iyelele mama eh
Mamee
Iyelele mama, iyelele mama, iyelele mama eh
Iyelele mama, iyelele mama, mamee aee
Lakini Mola muweza wa yote, wa yote
Kaninusuru na matatizo yamekwisha oh mama
Lakini Mola muweza wa yote, wa yote
Kaninusuru na matatizo yamekwisha oh mama
[Pre-Chorus]
Kweli nimekusamehe lakini sitokusahau
Na yaliyopita si ndwele tugange yajayo kaka
[Chorus]
Lalalalalalala lalalalala la
Lalalalalalala mimi nimekusamehe
Lalalalalalala lalalalala la
Lalalalalalala mimi nimekusamehe

SIKU HAZINGADI LYRICS BY LADY JAY DEE


[Chorus] x2
Yote mlosema, mlotenda, nasahau nasonga mbele
Mangapi yamesemwa, mangapi nimeona mh mliosema
Aah nasonga mbele
Mangapi yamesemwa, mangapi nimeona
Eh nimesemwa sana jamani, hamchoki?!
[Verse 1]
Nadhani hamyajali maumivu yangu moyoni
Na wala hampendi kwangu yatokee mazuri
Hata nisiowategemea, leo hii mmenigeuka
Hata nilio waheshimu, leo hii mnanihukumu
Kila mtu ana dhambi, msijihesabie haki
Kusemwa semwa sitaki, hakuna alie msafi
[Chorus] x2
Yote mlosema, mlotenda, nasahau nasonga mbele
Mangapi yamesemwa, mangapi nimeona mh mliosema
Aah nasonga mbele
Mangapi yamesemwa, mangapi nimeona
Eh nimesemwa sana jamani, hamchoki?!
[Verse 2]
Sijali maneno yenu kwani kuna hata magazeti
Sijali visa vyenu havifanii kwa ukweni
Ni potofu fikra zenu msokaa kufanya yenu
Kunijua sana undani siwapi tena nafasi
Ooh siku hazigandi, hata mseme mangapi
Kila mtu ana dhambi, hakuna alie msafi
[Verse 3]
Nadhani hamyajali maumivu yangu moyoni
Na wala hampendi kwangu yatokee mazuri
Hata nisiowategemea, leo hii mmenigeuka
Hata nilio waheshimu, leo hii mnanihukumu
[Chorus] x2
Yote mlosema, mlotenda, nasahau nasonga mbele
Mangapi yamesemwa, mangapi nimeona mh mliosema
Aah nasonga mbele
Mangapi yamesemwa, mangapi nimeona
Eh nimesemwa sana jamani, hamchoki?!

NILIAMUA LYRICS BY LADY JAY DEE

[Chorus] x2
Niliamua kukupenda wewe
Niliamua kuwa karibu nawe
Ya waswahili sikuyaendekeza
Nilijua wangetutenganisha
[Verse 1]
Ilikuwa ni maamuzi ya moyoni juu ya mapenzi
Natafuta njia nzuri tangu zile zetu enzi
Sababu mikosi tele imeniandama mithiri ya nyuki
Na nimeamua sitoweza saliti ndoa yetu mimi
Ni maamuzi toka ndani ya moyo niamini mpenzi
Nimechoshwa na lawama nafafia maradhi mimi
Ni kwamba mapema utahaha kutafuta mwingine mpenzi
Na sitoruhusu hiyo hali itokee ndani ya yako nafsi
Naogopa maradhi mimi, naogopa ngoma mimi
Naogopa maradhi mimi, jamani
[Chorus] x2
Niliamua kukupenda wewe
Niliamua kuwa karibu nawe
Ya waswahili sikuyaendekeza
Nilijua wangetutenganisha
[Verse 2]
Hapana nilikua yote haya sitoweza kuyaacha mpenzi
Geuka, tazama kitandani kadi ya kopa my sweety
Sasa niamini nichoshwa na siri ya maisha ya uhuni
Na ndio sababu sitoweza vunja moyo wako, abadani
Nahisi ni upumbavu kuwa kama vile nilivyokuwa eti
Na kama nilikuwa kiziwi basi si kiziwi tena mpenzi
Mpenzi nahofia unaweza achia ngazi mapema
Na sitoruhusu hiyo hali itokee ndani ya yangu nafsi
Hayo yote ni maamuzi niliochukua mwangu moyoni
Lengo langu ilikuwa kuyaenzi yetu mapenzi
Hayo yote ni maamuzi niliochukua mwangu moyoni
Lengo langu ilikuwa kuyaenzi yetu mapenzi
[Verse 3 – Lady Jay Dee]
Na leo my love nakuapia
Sitorudia yoyote nilokosa
Mapenzi nilio nayo ni ya kweli
Tudumishe tuwakomeshe wenye chuki
Nafsi yangu nakupa tena
Moyo wangu pia chukua
Penzi la milele liwepo baby
Sitokuacha milele, milele
Ninakikabidhi kifo oh
Utengano wangu na wewe
Ninamuachia Mungu
Kuamua wala sio walimwengu
Oh wabaya!
[Chorus] x3
Niliamua kukupenda wewe
Niliamua kuwa karibu nawe
Ya waswahili sikuyaendekeza
Nilijua wangetutenganisha