Showing posts with label BUSHOKE. Show all posts
Showing posts with label BUSHOKE. Show all posts

Wednesday, 20 July 2016

NALIA KWA FURAHA LYRICS BY BUSHOKE FT K-LYNN

[Chorus] x2
[Bushoke]
Mbona wanitazama, kisha waanza kulia?
Kama nimekukosea, naomba nisamehe
[K-Lynn]
Hapana hujanikosea, mi nalia kwa furaha
Mapenzi unayonipa, sijawahi kupata
[Verse 1 – K-Lynn]
Unaposogea karibu, unaponishika mkono
Unaponitazama machoni, nashindwa vumilia
Mapenzi unayonipa, sijawahi kupata
Najiuliza ni kwanini, hatukujuana mapema
Nimeishi na wasojua mapenzi
Wasojua hata kunyenyekea
Nimeishi na wanaojua ku-force
Wasojua hata kubembeleza
Ninapokuwa na wewe, najiona ndio mwenyewe
Hata kama sina pesa, najiona tajiri
Hata kama sijala, najiona nimeshiba
[Chorus] x2
[Bushoke]
Mbona wanitazama, kisha waanza kulia?
Kama nimekukosea, naomba nisamehe
[K-Lynn]
Hapana hujanikosea, mi nalia kwa furaha
Mapenzi unayonipa, sijawahi kupata
[Verse 2]
[K-Lynn]
Naomba Mungu atujalie, tufunge ndoa mi na wewe
Na watoto pia tuzae, wakuite baba na mi mama
Maisha yangu bila wewe, sawa na basi bila konda
Maisha yangu bila wewe, mbele sitosonga
[Bushoke]
Na bado, na bado, sijafika mwisho
Na bado, na bado, sijamaliza kitabu
Vumilia maisha yangu, utakula vya kwangu
Mimi si wale wanaojisifu kwa ngono
Mapenzi si maneno, mapenzi ni vitendo
Na bado, na bado, nimesema bado
[Chorus] x2
[Bushoke]
Mbona wanitazama, kisha waanza kulia?
Kama nimekukosea, naomba nisamehe
[K-Lynn]
Hapana hujanikosea, mi nalia kwa furaha
Mapenzi unayonipa, sijawahi kupata

MAPENZI YANA RAHA LYRICS BY BUSHOKE

[Chorus]
Kweli nimeamini (amini)
Mapenzi yana raha (yana raha)
Nimeamini mimi (oh mama)
Mapenzi ni matamu (ni matamu)
Anaesema shubiri (oh mama)
Huyo hayajui (hayajui)
Anaesema mabaya (oh mama)
Huyo ana matatizo (matatizo)
Ooh nimeamini (amini)
Mapenzi yana raha (yana raha)
Nimeamini mimi (amini)
Mapenzi ni matamu (ni matamu)
Anaesema shubiri (oh mama)
Huyo hayajui (hayajui)
Anaesema mabaya (mabaya)
Huyo ana matatizo (matatizo)
[Verse 1]
Sijahadithiwa mimi, naelewa
Oh sijasimuliwa mimi, naelewa
Mapenzi, mapenzi, mamaa
Mapenzi umpate anayependa
Mapenzi, mapenzi, yana raha
Mapenzi umpate anayependa
Kama mimi nampenzi, ananipenda sana
Mtoto wa kitanga jama
Ananipenda sana
Ananipa kila kitu
Hadi ambavyo sikuomba
Ananipa mambo yote
Hadi ambayo siyajui
Anionapo nawaza mimi, jamani eeh
Ye huja kuniuliza mama, jamani wooh
Anionapo nafuraha mimi, Bushoke jama
Yeye huridhika jama, oh mpenzi wangu
Nampenda sana jamani
Hata mseme nini leo
Nampenda sana mimi, oh jama nampenda
[Chorus]
Kweli nimeamini (amini)
Mapenzi yana raha (yana raha)
Nimeamini mimi (oh mama)
Mapenzi ni matamu (ni matamu)
Anaesema shubiri (oh mama)
Huyo hayajui (hayajui)
Anaesema mabaya (oh mama)
Huyo ana matatizo (matatizo)
Ooh nimeamini (amini)
Mapenzi yana raha (yana raha)
Nimeamini mimi (amini)
Mapenzi ni matamu (ni matamu)
Anaesema shubiri (oh mama)
Huyo hayajui (hayajui)
Anaesema mabaya (mabaya)
Huyo ana matatizo (matatizo)
[Verse 2]
Mi na wazo la kwenda, huko Amerika
Sina hata wazo mimi, la kwenda South Africa
Nikafanye nini huko? Mpenzi wangu yuko Tanzania
Nikafanye nini mimi? Mpenzi wangu yuko Tanzania
Sina wazo la kuishi Oysterbay mimi
Sina wazo la kuishi hata Masaki mimi
Nikafanye nini huko? Mpenzi wangu yupo Yombo Buza
Nikafanye nini huko? Mpenzi wangu yupo Yombo Buza
Nampenda jamani, mamaa jamani
Nampenda mimi, nampenda sana
Hakuna kitu kizuri, zaidi ya mapenzi
Hakuna kitu kizuri jama, zaidi ya mapenzi
Hata mafukara nao, wanahitaji mapenzi
Hata matajiri nao, wanataka mapenzi
Na mapenzi wanayotaka, ndio ninayopata mimi
Na mapenzi wanayotaka, ndio ninapata mimi
Nampenda mamii jama, nampenda mpenzi wangu
Hata mkisema nini, nampenda jama sana
Hata kama ye malaya, nampenda hivyo hivyo
Hata kama ye mbaya, ndicho nilichompendea mimi
Hata kama yuko vipi, naelewa mimi hihi
Uzuri wake, naelewa mimi hihi
Hata ubaya wake, nael–
Oh mamaa
[Chorus]
Kweli nimeamini (amini)
Mapenzi yana raha (yana raha)
Nimeamini mimi (oh mama)
Mapenzi ni matamu (ni matamu)
Anaesema shubiri (oh mama)
Huyo hayajui (hayajui)
Anaesema mabaya (oh mama)
Huyo ana matatizo (matatizo)
Ooh nimeamini (amini)
Mapenzi yana raha (yana raha)
Nimeamini mimi (amini)
Mapenzi ni matamu (ni matamu)
Anaesema shubiri (oh mama)
Huyo hayajui (hayajui)
Anaesema mabaya (mabaya)
Huyo ana matatizo (matatizo)

BARUA LYRICS BY BUSHOKE

[Chorus] x2
Leo nimepata barua kutoka kwa mpenzi wa zamani
Anasema eti ameli-miss penzi langu la thamani
Bushoke, nimepata barua toka kwa mpenzi
Yule yule, aloutesa moyo wangu
[Verse 1]
Ni mpenzi ambae tulipenda sana
Ila tulikuja tengana baada ye kwende Kenya kusoma
Nilitamani kwenda nae, ila uwezo mimi sina
Aliniahidi akirudi, nitafunga nae ndoa
Nilidhani ni kweli mamaa, kumbe alikuwa ananidanganya
Nilidhani ni kweli mamaa, kumbe alikuwa ananidanganya
Mimi oh, mimi
Miezi miwili tu kupita, akanijulisha kwa barua
Amepata bwana mwingine, na wanapendana sana
Miezi miwili tu kupita, akanijulisha kwa barua
Amepata bwana mwingine, wanataka funga ndoa
[Chorus]
Leo nimepata barua kutoka kwa mpenzi wa zamani
Anasema eti ameli-miss penzi langu la thamani
Bushoke, nimepata barua toka kwa mpenzi
Yule yule, aloutesa moyo wangu
[Verse 2]
Kama ilivo Mungu hamtupi mja wake, mama ah
Akanijalia nami nikapata bibi oh
Kama ilivo Mungu hamtupi mja wake, mama ah
Akanijalia nami nikapata mpenzi oh
Niliompenda, alienipenda
Niliemthamini, akanithamini
Mwenye kuninyunyiza marashi ya upendo oh
Na kunitoa shombo la uchumba hewa
Mwenye kuninyunyiza marashi ya upendo oh
Na kunitoa shombo la uchumba hewa
Sasa leo hii mamaa, leo hii mamaa
Nimepata barua toka kwa mpenzi wa zamani
Anasema ya kwamba anataka eti kuwa nami
Nitafanya nini mimi, nami na mpenzi sasa
Anasema eti Mungu anasamehe na mi nisamehe pia
Eti Mungu anasamehe, na mi nisamehe pia
Kumpenda bado nampenda, msema kweli mpenzi wa Mungu
Ila nachofikiria mimi ni mpenzi wangu wa sasa
Mimi oh… Bushoke
[Chorus] x2
Leo nimepata barua kutoka kwa mpenzi wa zamani
Anasema eti ameli-miss penzi langu la thamani
Bushoke, nimepata barua toka kwa mpenzi
Yule yule, aloutesa moyo wangu

MSELA JELA LYRICS BY BUSHOKE

[Verse 1]
Ilikuwa Jumapili tarehe 9
Ama hakika siku ya visitors
Nimem-miss msela wangu, masikani yetu Sinza
Tumefika mapaka pale, tukamuona afande
Na tulikuwa masela kama wanne
Tumepeleka mazagazaga kibao
Siwezi taja yaani yalikuwa kibao
Nilipomuona kwa mbali nilifurahi
Alipofika karibu I started to cry
Nilipomuona kwa mbali nilifurahi
Alipofika karibu I started to cry
Msela amechoka, msela amekonda
Ana mapele mwili mzima
Jama msela anateseka
[Chorus] x2
Nimetoka kumcheki msela jela
Amenipa ukweli kesi yake
Naongea kwa uchungu huku nalia
Watu wanaamini kesi yake
Na pia anawapa hi
Na pia anawasabahi
Na pia anawapa hi
Na pia anawasabahi
[Verse 2]
Msela kaniambia yeye hakukosa
Msela, ila ushahidi haukutosha
Msela kaniambia yeye hakukosa
Msela, ila ushahidi haukutosha
Msela tumuombee Mungu atatoka
Japo ataanza maisha upya
Hiyo sio mbaya ili mradi katoka
Msela kaniambia yeye hakukosa
Msela, ila ushahidi haukutosha
Msela tumuombee Mungu atatoka
Japo ataanza maisha upya
Hiyo sio mbaya ili mradi katoka
[Bridge]
Weyo weyo weyo (weyo)
Weyo weyo weyo (weyo)
Weyo weyo weyo (weyo)
Weyo weyo weyo (weyo)
Mama mama mama mama mama mae (mamae)
Mama mama mama mama mama mae (mamae)
Mama mama mama mama mama mae (mamae)
Mama mama mama mama mama mae
[Verse 3]
Hata kama nikifa, P atoke
Hata kwa msamaha wa raisi
Hata kama nikifa, P atoke
Hata kwa msamaha wa raisi
Raisi mtote P, watu wanampenda P
Raisi mtote P, watu wanampenda P
[Bridge]
Weyo weyo weyo (weyo)
Weyo weyo weyo (weyo)
Weyo weyo weyo (weyo)
Weyo weyo weyo (weyo)
Mama mama mama mama mama mae (mamae)
Mama mama mama mama mama mae (mamae)
Mama mama mama mama mama mae (mamae)
Mama mama mama mama mama mae (mamae)
[Chorus] x2
Nimetoka kumcheki msela jela
Amenipa ukweli kesi yake
Naongea kwa uchungu huku nalia
Watu wanaamini kesi yake
Na pia anawapa hi
Na pia anawasabahi
Na pia anawapa hi
Na pia anawasabahi

WANASHINDWA LALA LYRICS BY BUSHOKE

[Verse 1]
Watu wanachonga wanasema mengi mengi
Tena wanataka kuona meli haisongi
Yaani wanalonga, longa sana mengi sichongi
Kukupenda wewe inawachoma
Kukupenda wewe inawachoma mama
[Chorus]
Wanashindwa lala wakisema
Kukupenda wewe inawachoma
Wanashindwa lala wakisema
Kukupenda wewe inawachoma
[Verse 2]
Inawachoma sana hawajui hata ni vipi tulikutana
Wanashangaa kuona eti vile nakupenda sana
Nawashangaa hawa jama wanasema umenipeleka kwa sangoma
Hayo ya nini wakati mapenzi anapanga Maulana
Wameanza tena
[Chorus]
Wanashindwa lala wakisema
Kukupenda wewe inawachoma
Wanashindwa lala wakisema
Kukupenda wewe inawachoma
Kukupenda wewe inawachoma
Kukupenda wewe inawachoma
[Verse 3]
Inawachoma sana juzi nimekununulia doti ya khanga
Italeta uhasama siku nitakayo kununulia Bima
Wanakata matawi nimeshikilia mizizi na shina
Mama wewe ninavyokupenda muulize Mwakachila
[Chorus]
Wanashindwa lala wakisema
Kukupenda wewe inawachoma
Wanashindwa lala wakisema
Kukupenda wewe inawachoma
Kukupenda wewe inawachoma
Kukupenda wewe inawachoma
(Kukupenda wewe inawachoma) x6
[Chorus]
Wanashindwa lala wakisema
Kukupenda wewe inawachoma
Wanashindwa lala wakisema
Kukupenda wewe inawachoma
Kukupenda wewe inawachoma
Kukupenda wewe inawachoma

NINKUGONZA LYRICS BY BUSHOKE

[Verse 1]
Mimi bado, kukata tamaa
Mimi bado, kukata tamaa
Nimewatuma rafiki zako
Waje wakupe ukweli kuhusu mi
Nimewatuma rafiki zako
Waje wakupe ukweli kuhusu mi
We ndie nilekuchagua
Wa kuwa wangu wa maisha
Sababu ya mimi kukupenda
Ni roho yangu kukuchagua
[Chorus]
Baby I, nataka uelewe I love you
(Love you, love you, love you, love you, love you
Love you, love you, love you, love you)
Baby I, nataka uelewe I love you
Ompee bigonzo byawe
Nanyenda kushemereza
Ompee bigonzo byawe
Ninshaba, onshobokerwe ninkugonza
Nakupenda, nakupenda, nakupenda uh ooh
Na-ku-pe-nda, na-ku-pe-nda
[Verse 2]
Mimi bado, kukata tamaa
Mimi bado, kukata tamaa
Naelewa unaogopa kuchezewa
Lakini mi nimekuja kamili
Naelewa unaogopa kuchezewa
Lakini mi nimekuja kamili
We ndie nilekuchagua
Wa kuwa wangu wa maisha
Nafsi yangu inaniambia
Kwako sijakosea
[Chorus]
Baby I, nataka uelewe I love you
(Love you, love you, love you, love you, love you
Love you, love you, love you, love you)
Baby I, nataka uelewe I love you
Ompee bigonzo byawe
Nanyenda kushemereza
Ompee bigonzo byawe
Ninshaba, onshobokerwe ninkugonza
Nakupenda, nakupenda, nakupenda uh ooh
Na-ku-pe-nda, na-ku-pe-nda
Ompee bigonzo byawe
Nanyenda kushemereza
Ompee bigonzo byawe
Ninshaba, onshobokerwe ninkugonza
Nakupenda, nakupenda, nakupenda uh ooh
Na-ku-pe-nda, na-ku-pe-nda

DUNIA NJIA LYRICS BY BUSHOKE

Kila mwanadamu mapungufu yake ye
Ye mwenyewe, na Mola ndo anajua
Kila mwanadamu mabaya yake yeye
Ni ye mwenyewe, na Mola ndo anajua
Kila mwanadamu matatizo yake yeye
Ni ye mwenyewe, na Mola ndo anajua
Kila mwanadamu machungu yake yeye
Ni ye mwenyewe, na Mola ndo anajua
Jipe moyo, usikate tamaa
Kumbuka tunaishi kwa nguvu ya Mola
Jipe moyo, usikate tamaa
Kumbuka na wewe umeumbwa
Haya maisha yasijekukuchanganya
Ukaabudu wengine ukamuacha Mola
Wale wenye mali nyingi
Wanamuona alokosa kama mnyama (Mola wasamehe)
Na sisi masikini
Kutwa tunapishana kwa wanganga (Mola tusamehe)
Wanasiasa wanasababisha tunauana yoyo
Wenyewe kwa wenyewe
Familia zao, kwao, ziko salama yoyoyo
Si tunauana wenyewe, oh
Mola wasamehe
Wanadhurumu mafukara ikiwa wao matajiri yoyoyo
(Mola wasamehe)
Wanadiriki hata kuua ili wawe matajiri yo
Mola wasamehe
Dunia aa ahaa (tunapita wewe)
Pesa, magari, majumba, takataka zote (tutaacha)
Utavuna aa aah (ulichopanda wewe)
Kama ulipanda mema utakuta pepo (utavuna)
Kama ulipanda mabaya utakuta moto (utachomwa)
Wanadhani Mungu abagua tajiri na fukara
(Ye hana kubagua wote wake)
Wa Mungu wote mwendawazimu na timamu
(Ye hana kubagua wote wake)
Unadhani utaulizwa ulikuwa na magari mangapi!
Unadhani utaulizwa wewe ulikuwa nani duniani!
Unadhani utaulizwa baba yako nani au wewe nani!
Yesu masiha nabii, Issa amesema
Ndie amesema sio mi niliesema
“Tajiri kuona ufalme wa mbingu
Sawa ngamia apenye tundu la sindano”
Hakikisha mali zako za halali
Hakikisha unapenda nduguzo
Hakikisha unajua utu ni nini
Isije pesa zako mwenyewe zikakuchoma mwenyewe, we we we
Ee ee mama, ah dunia
Dunia aa ahaa (tunapita wewe)
Pesa, magari, majumba, takataka zote (tutaacha)
Utavuna aa aah (ulichopanda wewe)
Kama ulipanda mema utakuta pepo (utavuna)
Kama ulipanda mabaya utakuta moto (utachomwa)

MUME BWEGE LYRICS BY BUSHOKE

[Verse 1]
Nilikuwa na mpenzi wangu, nani asiyemjua
Mtoto kaumbika, utasema malaika
Miezi kadhaa ikasogea, mtoto wa kwanza tukazaa
Mtoto katoka mwarabu, swali lilikosa jibu
Akasema we hujui, mtoto kafata kwa babu
Nikaguna guna pale mzee, nikauchuna
Mtoto wa pili tukazaa, huyu wa sasa mchina, duh!
Nikasema mama vipi, mbona mi sielewi!
Akasema we hujui, huyu kafata kwa bibi
Mzee naibiwa, mzee naonewa
[Chorus] x2
Awe mama wee, ingekuwa ungefanyaje?
(Awe mama wee, ingekuwa ungefanyaje?)
Awe mama wewe, uwe ungefanyaje?
(Awe mama wee, ingekuwa ungefanyaje?)
[Verse 2]
Mwenzenu nalala chini, mke wange kitandani
Nikilala kitandani, kila mtu shuka lake
Mwenzenu nalala chini, mke wange kitandani
Nikilala kitandani basi ujue mzungu-wa-nne
Nikiuliza kwanini, anasema amenipa likizo eh
Nikiuliza kwanini, anasema amenipa likizo eh
Sio kama napenda, imenilazimu
Sio kama napenda, ananilazimisha yo
Mwenzenu naosha vyombo, mwenzenu napiga deki
Mzee mzima napika, jamani nafua nguo
Sio kama napenda, nalazimishwa mimi
Sio kama napenda, nalazimishwa mimi
[Bridge]
Uliniacha na mtoto wangu mdogo Vanessa eh
Miaka inakwenda, siku zinarudi mimi na Vanessa eh
Wewe utakuja nikumbuka
Wewe utakuja niuliza
Gigigi mapenzi na wewe sasa yamekwisha
Usinijue jue, usinitambue
Oh chunga nyumba na mama Vanessa eh
Oho chunga nyumba na mama Vanessa eh
Fadena mapambano yo
[Chorus] x2
Awe mama wee, ingekuwa ungefanyaje?
(Awe mama wee, ingekuwa ungefanyaje?)
Awe mama wewe, uwe ungefanyaje?
(Awe mama wee, ingekuwa ungefanyaje?)
[Outro]
Mke wangu mwanajeshi, mwenzenu nafua gwanda
Nikileta ubishi, ananipiga mashuti
Jana kaniambia eti nimsindikize gesti
Ila nimsubiri kwa nje eti anaenda kuongea mambo ya business
Ameenda kugombana na mashoga zake
Halafu ananiambia eti mi niende nikasute
Leo kanifukuza chumbani eti nitoke nje
Kisa anavaa nisije nikamchungulia