Showing posts with label matonya. Show all posts
Showing posts with label matonya. Show all posts

Monday, 25 July 2016

Vaileti lyrics by matonya

[Chorus]
Watu walishachonga sana
Eti Vailet simpati tena
Na kuongea uzushi bwana
Kwa kuona mambo yetu yananyooka
Hata kiss, hug sipati oh mama, baby
Watu walishachonga sana
Eti Vailet simpati tena
Na kuongea uzushi bwana
Kwa kuona mambo yetu yananyooka
Hata kiss, hug sipati oh mama, baby
[Verse 1]
Mi na huyu demu tunapendana
Sisi kila sehemu mimi naye hatutoachana
Kwenye shida na raha sisi tunapendana
Bora tunapendana
Mseme msemavyo tutazikana
Mi na Vai hatutoachana
Mbane mbanavyo tutazikana
Mi naye hatutoachana
Wanaogombana wanapatana
Nikikuudhi naomba unisamehe
Kama kadi I’m sorry mpenzi nikuletee
Semaa unachotaka
Chochote unachotaka nitakupa maa
Baby usiwe na pupa
usiwe kama fisi unataka mfupa
Wewe Vailet amini we ndo
My sweet heart, mi napenda unavyodeka
Unavyocheka, mwili unaweweseka
[Chorus]
Watu walishachonga sana
Eti Vailet simpati tena
Na kuongea uzushi bwana
Kwa kuona mambo yetu yananyooka
Hata kiss, hug sipati oh mama, baby
Watu walishachonga sana
Eti Vailet simpati tena
Na kuongea uzushi bwana
Kwa kuona mambo yetu yananyooka
Hata kiss, hug sipati oh mama, baby
[Verse 2]

Vailet njoo Vailet usihofu
Vailet usifanye chochote itakuwa soo
Kwani mi mwenzako Tonya nakupenda sana
Ziba masikio wanafiki watakudanganya
Vailet basi usiwe na wasi
Ushanikataza nastop kuvuta nyasi
Kuna mazuri baby utakuwa huyapati
Kipindi kile we utaponisaliti we
Vailet we ndo keki wengine fake
Wataolewa hawariziki we
Mi na wewe tu, we ndo wangu sista duu
Usiwe na makuu nasisitiza we ndo my au
Vailet usininyanyase mie
Vailet nini nikununulie
[Chorus]
Watu walishachonga sana
Eti Vailet simpati tena
Na kuongea uzushi bwana
Kwa kuona mambo yetu yananyooka
Hata kiss, hug sipati oh mama, baby
Watu walishachonga sana
Eti Vailet simpati tena
Na kuongea uzushi bwana
Kwa kuona mambo yetu yananyooka
Hata kiss, hug sipati oh mama, baby

Dunia Mapito lyrics by Matonya

[Verse 1]
Aah dunia
Bado nikiza, bado nikiza
Na marashi ya dunia siyasikii
Najihisi nipo kuzimu naishangaa sayari hii
Iliyojawa wanasiasa, michezo na wasanii
Najiuliza wamekuja huku kutalii
Au wameshahamia dunia ndo haijirudii?
Mara nasikia swali kama la nguvu za hoja
Dandu ananiuliza ‘albamu zinajikongoja?
Vipi mmegonga copy chini ya milioni moja?’
Jibu zinalipa sio moja kwa moja
Steve 2K anauliza ‘bifu zinaendeleaje?
Nimesha msamehe Casto ameshatoka Segerea?’
Namjibu bifu lipo na vita vinanyongea
Casto bado anaoza, tuanzeni kumuombea
Complex naye anauliza ’albamu ile ya wagosi
Walishagonga kopi ngapi hadi sasa kwa wadosi?
Namjibu tangu ufe mambo yote ni mikosi
Makundi yanavunjika duniani tunakumiss
[Chorus]
Yee iye iye eh
Dunia mapito jamaa
Tuwaombeeni waliokufa wende salama
Mi nawe tupo hatujui siku yetu lini
Kinachotakiwa tuishi kwa amani duniani (mi na wewe)
Yee iye iye eh
Dunia mapito jamaa
Tuwaombeeni waliokufa wende salama
Mi nawe tupo hatujui siku yetu lini
Kinachotakiwa tuishi kwa amani duniani
[Verse 2]
Kulia nafuta chozi, kushoto lanidondoka
Nakosa raha TX Moshi nikimkumbuka
Muone ananiuliza ‘muziki wa dansi ndio ushashuka?’
Jibu bado upo, ila naamini pengo lako halitozibika
Mara kwambali nasikia sauti ya gitaa
Sauti ya gitaa inapigwa huku inaniita
Kumbe mzee wakale, hayati Bob Marley
Ananiuliza ‘mziki wa Reggae unaenda vipi?’
Reggae bado ipo
Ziggy na Damian na Jissy wanagonga copy
Marijani, ananiuliza ‘muziki wangu unaimbwa sana duniani
Vipi familia yangu inafaidika kitu gani?’
Jibu mimi sina labda mwanao Marijani
Kiza ni kinene sioni pa kupapasa
Mara kwa mbali nawaona wanasiasa
Machozi yananitoka, chini nadondoka
Namuona Karume na Nyerere Julius
Wananiuliza ‘muungano je una nafasi?’
Nawajibu msiwe na wasi
Sasa ari mpya, nguvu pia na kasi
Ulimwengu mmeuacha dunia ndio inawamiss
[Chorus]
Yee iye iye eh
Dunia mapito jamaa
Tuwaombeeni waliokufa wende salama
Mi nawe tupo hatujui siku yetu lini
Kinachotakiwa tuishi kwa amani duniani
Yee iye iye eh
Dunia mapito jamaa
Tuwaombeeni waliokufa wende salama
Mi nawe tupo hatujui siku yetu lini
Kinachotakiwa tuishi kwa amani duniani

Anita lyrics by Matonya ft Lady jay dee

Chorus – Matonya]
Anita (iye iyee)
Anita wangu (uwo uwo)
Lelele lilele iye iyee
Nasukuma sukuma, ili siku ziende
Urudi nyumbani tuishi pamoja
[Verse 1 – Matonya]
Nasikia mazoea yanatabu, leo ndio naamini
Tangu uondoke Anita raha nakosa mimi
Hukumbuki tulilishana yamini
Kwamba mimi na wewe
Maisha milele mpaka nafukiwa chini
Ni mawazo yanautesa moyo wangu Anita nielewe iyee
Natamani uyajue ili unilinde mimi
Sijajua uliwaza nini Anita kuwa mbali na mie iyee
Hata hilo nilijue ili nisaishwe mimi
Kama ni maradhi, mimi ndio wako dakitari
Unambie mapema ili dawa yake niijue
Ama ni waradhii iiih hiii
Anii..
[Chorus – Matonya]
Anita (iye iyee)
Anita wangu (uwo uwo)
Lelele lilele iye iyee
Nasukuma sukuma, ili siku ziende
Urudi nyumbani tuishi pamoja
[Verse 2]
[Lady Jay Dee]
Unajua mi nilikupendaa zaidi
Ila ya dunia we yalikuzidi
Nilitamani kuwa nawe zaidi
Kuliko yoyote unayemdhani
Siku zote uko safarini kuniacha mimi upweke
Mi nilikupenda sana we mpenzi
Je kweli wataka kunienzi?
Au unataka kunitia mi mashakani?
[Matonya]
Siku zaenda kama chizi, ni yangu njiani naongea
Hiyo yote sababu yako Anita kilio pokea
Chefu na majirani mtani wanakuulizia
Sina la kuwajibu nabaki kama chizi najililia
Waliniambia nikuache wewe
Ili mi niishi mwenyewe
Masikio nikaziiba, vipi niishi bila wewe
Wakasema hutonithamini, wala haikuniingia akilini
Mbuzi gita wakapiga jua wewe ndio wa maishani
Anita wewe umeumbika mama
Kila upitapo nyuma lawama
Sijiwezi mtoto wa kitanga
Kwako taabani nishabwaga manyanga
Anita wewe umeumbika mama
Kila upitapo nyuma lawama
Sijiwezi mtoto wa kitanga kwako taabani
Anita, nakuita..
[Chorus – Matonya] x2
Anita (iye iyee)
Anita wangu (uwo uwo)
Lelele lilele iye iyee
Nasukuma sukuma, ili siku ziende
Urudi nyumbani tuishi pamoja
[Outro]
Pamoja, pamoja na Dunga
Ndani ya 49 Records
Pamoja iih na Jide (aan haa, ah Jide)
Mkata, ndani ya 49 Records (oh pamojaa!)

Taxi Bubu lyrics by matonya ft Fid Q

[Intro – Fid Q]
Kumbe ni taxi bubu, niliemuhusudu
Akaniganda mithiri ya mdudu kupe
Mchana za njano, usiku ana nyeupe
Yaliyomo hayamo, lakini nimeona it’s not fair
[Verse 1 – Matonya]
Kweli usilolijua usiku wa giza
Kipenzi cha moyo leo hii kinaniliza mimi
Hisia nilimpa yeye sababu ya kumuamini
Ni chunusi si baharini, hata nchi kavu pia jamani wanathamani
Mwenzenu nkasema labda nionapo picha ya kimwana mi ni hoi
Kumbe sivyo bwana, vile nilivyodhani awe wangu wa milele
Hivi ndivyo alivyo kupenda anataka, kupendwa anaogopa
Sababu ana mengi maovu asije umbuka
[Chorus – Matonya] x2
Kumbe taxi bubu mchana namba za nyano, usiku weka nyeupe
Na mi Tonya nishamuhusudu nae kaniganda ganda mithiri ya mdudu kupe na..
[Verse 2 – Matonya]
Ni bora ningejua mapema kama maisha yako wewe ni ya viwanjani
Sio ufala, ulinizuga sana kwamba wewe huna hizo ni wa getini
Mchana unakuja home mitandio kichwani
Usiku ndo sikuoni

Kumbe mwenzangu mimi kiwanja Kinondoni kwa Macheni hamjui nani!
Usiwaone tu machoni, jua kuna wengine mazugoni maofisini
Kumbe nao hao (kuwa nao)
Kumbe nao hao (cheka nao)
Kumbe nao hao..
[Chorus – Matonya] x2
Kumbe taxi bubu mchana namba za nyano, usiku weka nyeupe
Na mi Tonya nishamuhusudu nae kaniganda ganda mithiri ya mdudu kupe na..
[Bridge – Matonya]
Muamini akuamini, umvike madini
Mkale kiapo mpaka mwafukiwa aridhini
Sio kichochoroni, kavu kavu mdomoni
Kakudanganya kuwa anaishi getini
Hupatikana hata mitaani ukimwi
Usimuamini kwa kumuona kwa macho
[Chorus – Matonya] x2
Kumbe taxi bubu mchana namba za nyano, usiku weka nyeupe
Na mi Tonya nishamuhusudu nae kaniganda ganda mithiri ya mdudu kupe

spare tairi lyrics by matonya


[Verse 1]
Najua nishachelewa
Kama kupenda umeshawahiwa
Nahisi kama ngekewa
Hadithi nzuri nasimuliwa
Kweli Maanani kaumba dunia kwa uwezo wa pekee
Nakupa marks asilimia mia baada wifey wewe
Kwani, lini, honey utakuja niamini?
Ya kwamba kidole kimoja hakiwezi vunja chawa hasirani
Pini ukinilia mi utanipa kovu kubwa maishani
Kwani Tonya mi tayari kuwa hata kwa spare tairi
[Chorus]
Tafadhali Lati niamini
Nenda kwanza kafikiri
Tonya boy mi ni tayari kuwa hata spare tairi
Bumsara bumsara ise (eeh!)
Hata maua hunyauka (eeh!)
Tafadhali Lati nitunze (eeh!)
Ipo siku ntakayofaa (eeh!)
Bumsara bumsara ise (eeh!)
Hata maua hunyauka (eeh!)
Tafadhali Lati nitunze (eeh!)
Ipo siku ntakayofaa (eeh!)
[Verse 2]
Kila ndege hutua kwenye mti aupendao
Hata kama una miba na majani kibao
Nishatota nugu tafadhali nikubali mwenzio
Hata kama una mchumba sitoweka vikwazo
Ayaa, hata mimi nakupenda kwenye hii sayari
Ayaa, na tabia za watu Lati huwezi tabiri
Unaweza tendwa na uliye nae
Nikaziba pengo juu yake yeye, Lati niamini
[Chorus]
Tafadhali Lati niamini
Nenda kwanza kafikiri
Tonya boy mi ni tayari kuwa hata spare tairi
Bumsara bumsara ise (eeh!)
Hata maua hunyauka (eeh!)
Tafadhali Lati nitunze (eeh!)
Ipo siku ntakayofaa (eeh!)
Bumsara bumsara ise (eeh!)
Hata maua hunyauka (eeh!)
Tafadhali Lati nitunze (eeh!)
Ipo siku ntakayofaa (eeh!)
[Bridge]
Kila kukicha mi naona jii
Hata mwenzangu hueleweki
Na jibu langu hunipi
Nitafanyanini sasa wangu Lati
Kila kukicha mi naona jii (eeh!)
Hata mwenzangu hueleweki (eeh!)
Na jibu langu hunipi (eeh!)
Nitafanyanini sasa wangu Lati (eeh!)
[Chorus]
Tafadhali Lati niamini
Nenda kwanza kafikiri
Tonya boy mi ni tayari kuwa hata spare tairi
Bumsara bumsara ise (eeh!)
Hata maua hunyauka (eeh!)
Tafadhali Lati nitunze (eeh!)
Ipo siku ntakayofaa (eeh!)
Bumsara bumsara ise (eeh!)
Hata maua hunyauka (eeh!)
Tafadhali Lati nitunze (eeh!)
Ipo siku ntakayofaa (eeh!)