Showing posts with label MARLAW. Show all posts
Showing posts with label MARLAW. Show all posts

Friday, 22 July 2016

RITA LYRICS BY MARLAW


[Chorus]
Sauti inasikika
Tega makini, hujui nani inamwita
Chozi lanitoka
Nitazamapo angani, naona sura ya Rita
Ona mikono yangu mitupu
Imezoea kukushika we
Hata nyumbani kwangu haupo
Umepotea sikuoni kwamwe
Ooh Rita, ooh Rita
Daily nakuwaza wee
Ooh Rita, ooh Rita
Mimi nitanyamazaje?
[Verse 1]
Rita we unajua jinsi gani mimi na wewe tulivyopendana
Jitoa sadaka kimapenzi ili mradi tusijetengana
Ila we unajua ni yako familia
Damu yangu ya Bongo si ya Asia
Ndo kigezo cha wao kunitosa
Mara mbili risasi wamenikosa
Kumbuka ile mimba ndio iliyokufanya ukaja kwangu (ulifukuzwa kwenu)
Ulijifunguapo mtoto na wote mkaishi kwangu (ukawachukiza kwenu)
Na taarifa ikaja kwako wewe Rita
Uende Arusha nduguzo wanakwita
Ukani-kiss kiss mimi na mtoto,
Nikaku-kiss ee eehee
[Chorus]
Sauti inasikika
Tega makini, hujui nani inamwita
Chozi lanitoka
Nitazamapo angani, naona sura ya Rita
Ona mikono yangu mitupu
Imezoea kukushika we
Hata nyumbani kwangu haupo
Umepotea sikuoni kwamwe
Ooh Rita, ooh Rita
Daily nakuwaza wee
Ooh Rita, ooh Rita
Mimi nitanyamazaje?
[Verse 2]
Ni tangu Arusha hadi Iringa simu inaita unapokea unalia
Kurudi Iringa uishi nami ndugu zako wamekuzuia
Ukasema laiti ungejua
Usingekubali uondokee pekee
Mwanao analia
Ona mumeo ni bora ninywe pombe
Ila kwa penzi uka-force kurudi
Piga simu mume wangu nakuja
Na maneno ya konda kwenye basi ulifika
Alikupa siti ukakaa, ulipokaa ukakaa
Ile siku mi nimelelewa
Niko mi na mwanangu, kumpokea mke wangu
Konda akasema si wewe, ila tu mwili wako
[Chorus]
Sauti inasikika
Tega makini, hujui nani inamwita
Chozi lanitoka
Nitazamapo angani, naona sura ya Rita
Ona mikono yangu mitupu
Imezoea kukushika we
Hata nyumbani kwangu haupo
Umepotea sikuoni kwamwe
Ooh Rita, ooh Rita
Daily nakuwaza wee
Ooh Rita, ooh Rita
Mimi nitanyamazaje?
Ooh Rita Rita ahh
Na Marco Chali
Ndani ya MJ Records
This is true story to Marco
Rita, Rita, Rita
Aaah hata nyumbani kwangu haupo!

BADO UMENUNA LYRICS BY MARLAW


[Verse 1 – Marlaw]
Najiuliza vipi kuhusu kosa
Vile mpenzi bado umenuuuna
Usiku na mchana we una hasira
Najiuliza kama utanitosa, sipati picha
[Pre-Chorus – Marlaw]
Mmh!
Bado umenuna, na hucheki tena
Najuta naogopa, roho inaniuuuma
Kosa ni kosa ukishakosa tena
Naomba samahani, mtoto mzuri sana
[Chorus – Marlaw]
Kwani sio langu kusudio, we uumie
Vile umenuna unaniweka roho juu baby
Hofu nilonayo mi mwenzio, nihurumie
We nisamehe kwani nipo nawe tu baby
Baby eh, baby eh
Tu baby eh, baby eh, baby ee
[Verse 2 – Chidi Benz]
Usinune
Nakubali nimekosa na sitokosa tena naapa hak’ya Mungu eeh
Upweke umenikaba na namiss mapenzi nayakumbata machungu ooh
Njoo, njoo ntapiga magoti
Sitolikwepesha shavu nipige hata makofi no!
Sina tena ukorofi ni..nitatii amri mi karaka we ndo bosi
[Pre-Chorus – Marlaw & (Chidi Benz)]
Bado umenuna (bado umenuna)
Na hucheki tena (ooh oh oh)
Najuta naogopa (najuta naogopa)
Roho inaniuuuma (braa bra bra bra bra)
Kosa ni kosa (jyeah ah)
Ukishakosa tena (si si si si si)
Naomba samahani (ah ah ah ah ah)
Mtoto mzuri sana (ooh)
[Chorus – Marlaw]
Kwani sio langu kusudio, we uumie
Vile umenuna unaniweka roho juu baby
Hofu nilonayo mi mwenzio, nihurumie
We nisamehe kwani nipo nawe tu baby eh
Baby eh, baby eh
Tu baby eh, baby eh, baby ee
[Verse 3 – Marlaw]
Elewa baby nachosema ah ah ah ah
Mmh napiga magoti, naomba msamaha
Kwamba baby, mi sitorudia tena ah mmh
Ehee (oohoo)
Si umenisamehe mama? (ooh)
Mmh si umenisamehe mamaaa mmh
Si umenisamehe mama eeh ee
Mmh si umenisameheeee eeeh
[Chorus – Marlaw]
Kwani sio langu kusudio, we uumie
Vile umenuna unaniweka roho juu baby
Hofu nilonayo mi mwenzio, nihurumie
We nisamehe kwani nipo nawe tu baby eh
Baby eh, baby eh
Tu baby eh, baby eh, baby ee
[Outro]
Oh uuh
Ooh mama
Lala lala mamaa ah
Oh eehaa (Marlaw)
Chi Chi Chidi Chichi Chidi Benz!
La Familia aah
Mapigo!
Sema mama (sema mama)
Marlaw
Mama ntapiga magoti, sina ukorofi
Jyeah oh
One love, dedication to all the girls
I see you, Marlaw!
Allan Mapigo, Chidi Benz, Marlaw!
Mwah mwah mwah

BEMBELEZA LYRICS BY MARLAW


[Chorus]
Hey hey hallo ma
Laiti ungekuwa unaniona
Vile kila time nakonda nawaza
Kama kukupata nitaweza
Jinsi gani kukueleza
Au mi sijui bembeleza
Usinikatae utaniumiza
Nakupenda kukutenda sitoweza
[Verse 1]
Kila time nakuangalia usoni ma
Sio kamaa nakosa neno kusema
Ulivyo ma anafanya kosa kunena
Ingawa moyo hautaki kunena tena
Wazo kichwani lina beep (kukueleza)
Ilavibaya ukinijibu (bembeleza)
Nahisi sijui bembeleza
Utakataa halafu mi utaniumizaa
Kidesign nakuangalia usoni ma
Kuna sign za kuita huko machoni ma
Kitu fulani umehifadhi huko moyoni ma
Unachotaka nianze mikusema
Hapa unafanya nijione (nitashinda)
Hapa unafanya nitamke (nakupenda)
Ilaunacho jibu mdomoni nitofauti nausemacho machoni
[Chorus]
Hey hey hallo ma
Laiti ungekuwa unaniona
Vile kila time nakonda nawaza
Kama kukupata nitaweza
Jinsi gani kukueleza
Au mi sijui kubembeleza
Usinikatae utaniumiza
Nakupenda kukutenda sitoweza
Hallo ma
Laiti ungekuwa unaniona
Vile kila time nakonda nawaza
Kama kukupata nitaweza
Jinsi gani kukueleza
Au mi sijui kubembeleza
Usinikatae utaniumiza
Nakupenda kukutenda sitoweza
[Verse 2]
Kati yetu imetawala rangi ya pinki
Kitu ambacho moyoni siridhikii
Nacho kuomba tuwe zaidi ya marafiki
Inajionyesha machoni unaafiki
Lugha ya macho kwa sasa (nakataa)
Tataka tuongee ilitufikie (mwafaka)
Kwenye party ulikuja umependeza
Kwenye traini ukaniomba mi kucheza
Tuka-dance na macho umelegeza
Ulinibamba nikaficha kukueleza
Unanimaliza, mimi ninakweleza, ninakubembeleza
Baby please baby girl
Vile unatamka, wewe kuona nataka, tuonge ana kwa ana,
Baby please baby girl
[Chorus]
Hey hey hallo ma
Laiti ungekuwa unaniona
Vile kila time nakonda nawaza
Kama kukupata nitaweza
Jinsi gani kukueleza
Au mi sijui kubembeleza
Usinikatae utaniumiza
Nakupenda kukutenda sitoweza
Hallo ma
Laiti ungekuwa unaniona
Vile kila time nakonda nawaza
Kama kukupata nitaweza
Jinsi gani kukueleza
Au mi sijui kubembeleza
Usinikatae utaniumiza
Nakupenda kukutenda sitoweza

PII PII LYRICS BY MARLAW


[Verse 1]
Ninataka niwahi kufika
Njia inajam sasa wapi nitapita
Nimekaa karibia saa sita
Sasa kukaa nimechoka oh baby
Sijamwona long time now
Nimerudi toka mwezi jana
Nimeshakwambia mama nimefika tangu mchana
Anajua nimeshafika, ameshapika, amekasirika
Alipika tangu mchana, ila sasa lunch imegeuka dinner
[Chorus]
Nimechoka kupiga honi now (pii pii), hatuelewani
Nimechoka kupiga honi now (pii pii), hatuelewani
Pii pii! Move out of the way, nimechoka kupoteza time
Nina siku nyingi kwenda home, I am missing my baby
Pii pii! Hello baby, natamani niwe nyumbani
Nimekwama hapa njiani, kuna jam baby
[Bridge]
Ah ah, kuna jam baby
Ah ahh, hello
Ah ahh, hello
Ah ahh, hello
[Verse 2]
Unanikatia simu unanionea
Wewe ungekuwepo ungejionea
Unafanya hivyo unakosea mamaa
Unanikatia simu unanionea
Wewe ungekuwepo ungejionea
Unafanya hivyo unakosea mamaa
Nakuomba mpenzi ungojee
Ni njiani naja niombee
Nimechoka nakuja tule, huruma nionee
Nakuomba mpenzi ungojee
Ni njiani naja niombee
Nimechoka nakuja tule, huruma nionee
[Bridge 2] x2
Nimechoka kungoja highway
Nitapita popote imradi wee
Ili kama ni kesi na iwe (pii pii, hatuelewani)
[Chorus]
Nimechoka kupiga honi now (pii pii), hatuelewani
Nimechoka kupiga honi now (pii pii), hatuelewani
Pii pii! Move out of the way, nimechoka kupoteza time
Nina siku nyingi kwenda home, I am missing my baby
Pii pii! Hello baby, natamani niwe nyumbani
Nimekwama hapa njiani, kuna jam baby
[Bridge 1]
Ah ah (oh), I love you so much
Ah ahh, I love you mama
Ah ah, I love you mamaa
[Bridge 2] x2
Nimechoka kungoja highway
Nitapita popote imradi wee
Ili kama ni kesi na iwe (pii pii, hatuelewani)
[Chorus]
Nimechoka kupiga honi now (pii pii), hatuelewani
Nimechoka kupiga honi now (pii pii), hatuelewani
Pii pii! Move out of the way, nimechoka kupoteza time
Nina siku nyingi kwenda home, I am missing my baby
Pii pii! Hello baby, natamani niwe nyumbani
Nimekwama hapa njiani, kuna jam baby
[Outro]
I love you so much, I love you Mama
I love you mama
I love you so much, I love you Mama
I love you mama
My baby, my baby
My baby, my baby
My baby, my baby

SORRY SANA LYRICS BY MARLAW


[Intro]
Ayayayaa heey
Ayayayaa ayayaaya
[Verse 1]
Ningejua toka mwanzo we ulinipenda mi
Nisingewaza niliyowaza juu yako mamii
Ningejua ulitayari maisha yako we na mi
Nisingewaza labda we utaniumiza mi
[Pre-Chorus]
Nimetoka mbali mimi, na mapenzi nimeshalia
Maumivu yangu mimi, nikaelekeza kwako pia
Nikapuuza wema wako, labda pia we ni muongo
Nikaona ndo wale wale wakunitesa roho
[Chorus]
Sorry sana aah, sorry sana aah
Sorry sanaa we ni mpenzi wangu
Sorry sana aah, sorry sana aah
Sorry sanaa we ni mpenzi wangu
[Verse 2]
Nilishaapa sitoingia tena upenzini
Nikajiamini lazma nije niishi peke yangu
Ujio wako kwangu mi niliona ni utani
Nikaona labda uje unipe mi company tu
[Pre-Chorus]
Umenibadilisha mengi, umenisahaulisha mengi
Sikukudhamini mwanzo, nakulipiza kwa upendo
Nilipuuza wema wako, labda pia we ni muongo
Nikaona ndo wale wale wakunitesa roho
[Chorus]
Sorry sana aah, sorry sana aah
Sorry sanaa we ni mpenzi wangu
Sorry sana aah, sorry sana aah
Sorry sanaa we ni mpenzi wangu
[Verse 3]
I say, I love you and I need you
I love you, love you, nishike
Mapenzi ni mi na we, mimi sasa ninajua
Thamani ya mapenzi kwako wewe mi naijua
Umenitoa kwenye giza, umenieka kwenye mwanga
Na sasa ma baby, I love you so much
Eee iiii iihh
Eee iiii iihh
Eee eee eeh
Ooh ooh wewee
Wewe ma baby, mamii iii iiih
[Chorus]
Sorry sana aah, sorry sana aah
Sorry sanaa we ni mpenzi wangu
Sorry sana aah, sorry sana aah
Sorry sanaa we ni mpenzi wangu
[Outro]
Wewe ni mpenzi wanguuu uuh
Wewe ma babyyy iiih
Ooh uuuh wewe ma baby
Wewe ma love eeeh
Eeeh wewe ma baby
Wewe ma looove aah aaa eeh

BWAYUWAYU LYRICS BY MARLAW


[Intro]
Nakupenda wewe
And I love you baby
Usimsikize huyo
Nimekaa na mrembo
Nimekaa na mrembo
Nimekaa na mrembo
Nimekaa..
[Verse 1]
Nimekaa na mrembo nampanga vile nitamuoa
Kwani nimempenda siku nyingi ila nikashindwa kumwambia
Ungeniuliza bwana kwani mimi nimeongea nini
Ungeongeza umakini huyu mtoto asingenikimbia
Nina imani kama ananipenda kaniruhusu niende nijieleze
Nimtume ujumbe mbayuwayu, mbayuwayu ngo ngo ngo
Mbayuwayu mimi ninakutuma ukifika usiwe kama huyu
Ubishe hodi mbayuwayu, hodi ngo ngo ngo ngo ee yeah
[Chorus]
Jirani au mgeni au sivyo ndivo kwako naomba bisha hodi (ngo ngo ngo)
Mvamizi au mwizi au sivyo ndivyo kwangu naomba bisha hodi (ngo ngo ngo)
Hodi (ngo ngo ngo)
Hodi (ngo ngo ngo)
Hodi (ngo ngo ngo)
Piga hodi yeah
Eee unaongea sana
Hujauliza kwanza, umevamia!
[Verse 2]
Niliongea na mrembo (mrembo), mrembo kakubalia
Nikajiona cha zaidi mi sina (sina), sina cha kuzugia
Imeniumiza sana kwani wewe umeongea nini
Kwa jinsi ninavyokuamini sikuwaza ungeniharibia
Nina imani kama ananipenda kaniruhusu niende nijieleze
Nimtume ujumbe mbayuwayu, mbayuwayu ngo ngo ngo
Mbayuwayu mimi ninakutuma ukifika usiwe kama huyu
Ubishe hodi mbayuwayu, hodi ngo ngo ngo ngo ee yeah
[Chorus]
Jirani au mgeni au sivyo ndivyo kwako naomba bisha hodi (ngo ngo ngo)
Mvamizi au mwizi au sivyo ndivyo kwako naomba bisha hodi (ngo ngo ngo)
Hodi (ngo ngo ngo)
Hodi (ngo ngo ngo)
Hodi (ngo ngo ngo)
Piga hodi
Hodi (ngo ngo ngo)
Hodi (ngo ngo ngo)
Hodi (ngo ngo ngo)
Hodi eei yai
Eeih mbayuwayu uende
Ukamuite baby, na hodi ubishe
[Bridge 1]
Sema hodi, sema hodi
Ukiskia karibu, ingia
Sema hodi, sema hodi
Ukiskia karibu, ingia
[Bridge 2]
Mbayuwayu paa paa paa paa (nenda wewe)
Mbayuwayu paa paa paa paa (afadhali wewe)
Mbayuwayu paa paa paa paa (huyu bure)
Mbayuwayu paa paa paa paa (hodi ubishe)
Mbayuwayu paa paa paa paa (nenda mwambie)
Mbayuwayu paa paa paa paa (nampenda yeye)
Mbayuwayu paa paa paa paa (yeye pekee)
Mbayuwayu paa paa paa paa ee iih
[Chorus]
Jirani au mgeni au sivyo ndivyo kwako naomba bisha hodi (ngo ngo ngo)
Mvamizi au mwizi au sivyo ndivyo kwako naomba bisha hodi (ngo ngo ngo)
Hodi (ngo ngo ngo)
Hodi (ngo ngo ngo)
Hodi (ngo ngo ngo)
Hodi (ngo ngo ngo)
Hodi (ngo ngo ngo)
Hodi (ngo ngo ngo)
Hodi (ngo ngo ngo)
Hodi yeei aii
[Bridge 1]
Sema hodi, sema hodi
Ukiskia karibu, ingia
Sema hodi, sema hodi
Ukiskia karibu, ingia
[Outro]
Mbayuwayu paa paa paa paa (nenda wewe)
Mbayuwayu paa paa paa paa (afadhali wewe)
Mbayuwayu paa paa paa paa (huyu bure)
Mbayuwayu paa paa paa paa (mwambie aelewe)
Mbayuwayu paa paa paa paa (baby baby)
Mbayuwayu paa paa paa paa (nakupenda wewe)
Mbayuwayu paa paa paa paa (baby nielewe)
Mbayuwayu paa paa paa paa (nakupenda sana)