Showing posts with label professor Jay. Show all posts
Showing posts with label professor Jay. Show all posts

Monday, 25 July 2016

bongo Dar es salaam lyrics by professor jay ft lady jay dee

[Verse 1 – Professor Jay]
Yoh, yoh, yoh
Ndani ya Bongo mambo super hapana ubongo
Ingawa sometime Bongo chungu kama sifongo
Nafanya makaratee kama machinga mtaa wa Congo
Kimtindo mtindo nakata ngebe vimtima nyongo
Hapana matata kitu roho inapenda mtapata
Bongo Dar Es Salaama ni mpeto wa kutakata
Nenda viwanja vikali vya Bongo ustaajabu
Na pita Sleepway, Blue Pam au Mambo Club
Kama hujazoea unaweza ukavunja shingo
Mambo Isidingo watu mkononi Nokia bingo
Huwezi kujua yupi mtoto wa geti, yupi changu
Wote wanameremeta kama mamtoni mwanangu
Hizi zinapoyeyuka wabongo tunalia ukata
Subiri kichapo chake pale mbongo anapozipata
Mwendo wa kiti kirefu jirani na nyama choma
Na toto mbili tatu za geti au za kona
Hii watu wa Bongo tunasema napoteza mawazo
Lakini mara nyingi hutokea wakati unazo
Wakati wa dumba kali saa moja shuka utosini
Na kujifanya unawaza mambo mengi ya ofisini
Pitia pitia night kali mitaa ya Kinondoni
Kina dada poa nusu uchi fegi mdomoni
Na kama una gari watajazana madirishani wee
Mpaka ukose hewa wote wanataka hisani
Kwenye madaladala kuibiwa ni kawaida
Vaa cheni shingoni, saa mkononi utoe faida
Wacha dirisha wazi kisha ukatize Manzese
Ili uwape mateja mtaji waende chimbo wakatese
Rudi Mwananyamala oh! Mateja kibao
Katiza saa moja moja uone roba za mbao
Utaona kama mtoa roho yuko karibu yako
Ni kheri utoe chochote ili uokoe nafsi yako
[Chorus – Lady Jay Dee]
Bongo eh
Bongo Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Bongo Dares Salaam
Kaa chonjo eh
Ndani ya Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Ndani ya Dares Salaam
[Verse 2 – Professor Jay]
Bongo ya sasa sio ya mwaka 47
Mpaka bibi vizee sasa wanafanya ukahaba
Sijui niseme nini ili muweze kunielewa
Na sijui nifanye nini nisaidie wanaoonewa
Hakuna heshima, ni vurugu mechi kwenye jamii
Hakuna utii wala mafunzo ya manabii
Na wezi wa mfukoni wanachomwa moto kinyama
Mwingine hajaiba kapewa kesi kwa uhasama
Nani atakae jua na sheria ipo mikononi?!
Watu wa Bongo mbona hamna utu moyoni
Vijana wamejibana wapate mtaji wa biashara
Nawaita machinga ingawa sio wote kutoka Mtwara
Mbaya kuliko vyote mnapovunja vibanda vyao
Wengine walikuwa wezi, je warudie zama zao?
Ni mshike mshike sometime ni vita na mapolisi
Wao na sisi, rungu na pingu kama ibilisi
Huku kwetu uswahilini ni mambo ya kila siku
Na ni kama kuibiwa cheni kwenye ngoma za mchiriku
Wabongo wanapenda sana starehe kuliko kazi
Wanatamani wangezaliwa Blue Nay wamwage radhi
Masista duu wa Bongo wanazidi kupanda chati
Huwezi kujua yupi wa Kigogo, yupi wa Masaki
Mablaza majina yao ya asili hawayataki
Bitoz Nyangema anataka aitwe Tupac!
Ni burudani tosha, hivyo ni vijimambo tu
Wabongo tuna title kubwa lakini hatuna kitu
Unaujua mstakabari wa ma-superstar wa Bongo?
Lazma ufunzwe chuo kikuu cha mbwembwe za uongo
City center, ofisi ni mtu aliposimama
Hata muhuri wa ikulu unapata haina gharama
Ngoma inakuwa nzito mnapokutana matapeli
Akili kumkito ukilemaa umeachwa ferry
Aliyeuziwa cheni katoa hela bandia
Aliyepokea hela nae kauza cheni ya bandia
Tuliozoea jiji tunasema ngoma droo
Na una-set mambo mengine yaende kwenye mtandao
[Chorus – Lady Jay Dee]
Bongo eh
Bongo Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Bongo Dares Salaam
Kaa chonjo eh
Ndani ya Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Ndani ya Dares Salaam
[Verse 3 – Professor Jay]
Katikati ya jiji hata usikiri dili haziji
Na ukitaka ku-win Bongo cheza dili na wale magwiji
Naona vijana wa Bongo wanapenda safari kafiri
Hata mkoba wanategua kitendawili
Safari bado ni ngumu jamani msiende kwa nguvu ya ndumba
Ujinga sumu acha Mwenyezi awahukumu
Changa uchange uende kiwanja unachotaka
Funga mkanda, fungua mabano unavyotaka
Maskani Kimara, watu kila siku magoni
Jonas Kiwia wasalimie Washington
Ukiweza pita Texas mpe hi Chief Son
Na mkumbushe uzushi wa Bongo Dar es Salaam
Sinza ya leo, kila baada ya nyumba bar
Na zote zinajaa, hapo ndipo utakaposhangaa
Na kwenye night club ni lundo la kaka poa
Huwezi ukaamini jinsi walivyojipodoa
Upinzani wa jadi Bongo haupo Simba na Yanga
Matonya na Makamba, na Sitte na wamachinga
Na kali kuliko zote upinzani konda na denti
Wanaposhika mashati tu denti anapoketi
Hakuna mnyonge, wala anayekubali kushindwa
Ngoma ngoroigwa na wote wanataka ubingwa
Na watu wana magari mpaka ya milioni 200
Kwa mbongo wa kawaida baiskeli kitendawili
Wasioamini ni wale wenzangu na mimi
Mlio na imani iliyopo juu mngoje chini
Mtangoja milele, na mtakufa bila kelele
Kama walivyokufa wafuasi wa Kibwetele
Ndani ya Bongo!
[Chorus – Lady Jay Dee] x2
Bongo eh
Bongo Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Bongo Dares Salaam
Kaa chonjo eh
Ndani ya Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Ndani ya Dares Salaam

Tathmini lyrics by professor jay ft jay more

[Verse 1 – Professor Jay]
Naahidi kuwa makini mpaka siku nafukiwa chini
Na Mungu aliye hai bado yu pamoja na mimi
Emcee shika vizuri karibu tawi linakatika
Na kwa wote mliopo juu na chini sauti itafika
Kazi na dawa ndani ya uswazi kazi ni kazi
Na nipo radhi kutoa tathmini ngazi kwa ngazi
Rap si lelemama kama wengi mnavyodhani
Fasihi iliyo hai kuitoa jamii gizani
Miaka ya 80 Hip Hop Bongo ilichipua
Na nadhani wale wakongwe wa rap hii mnaitambua
Hali ilikuwa mbaya miaka ya 89
Watu hawakutaka kuelewa rap kabisa
Miaka ya 90 Hip Hop Bongo imekubalika
Wenye nia nzuri na rap tunawajibika
Rap ni wito yataka utashi na ufahamu
Elimu ya mtaani kujituma pia nidhamu
Wasanii wenyewe wa Bongo tunaofanya tudharauliwe
Watu vibongo vidogo hawataki washauriwe
Wanaongea blah blah, vijino viwe
Na wanaovunja hata miko ya rap waheshimiwe!
Wengine watatumia kivuli cha rap kufanyia uhuni
Hii ni sawa na kupanda ngazi kuelekea mbinguni
tathmini ya kweli yatia majaribuni
Na mnaovunja miko ya rap jihukumuni
[Hook – Professor Jay] x2
Hii ni tathmini kwa wote juu na chini
Yoh emcee zunguka nyuzi 360
Umeona nini? Mwana mpotevu rudi kundini
Fani ni uwanja mpana na jua lipo utosini
[Verse 2 – Jay Moe]
Yoh! Mawazo ya Jay Moe usiku mchana yalikuwa wima
Ingawa sikujua usiku ukiisha asubuhi itakuwa neema
Kwani baba mama miaka ile kipindi cha nyuma
Waliamini rap ni kuimba yale yasiokuwa mema
Haina noma wakwezi tulipomaliza kusoma
Mistari iliandikwa ujumbe ukashuka ukakubalika
Ndio ilikuwa bado wenye hisa kutolea macho
Walithamini Bolingo, ambacho kimewachosha Bongo
Wahisani waongo, walidhani tungedorola
Mara ngoma ika-change na nyota ya rap ikang’ara
Wasambazaji habari ya kwamba Hip Hop uhuni
Wameingia mitini ‘Chemsha Bongo’ ilipoingia redioni
Kama wametawala ikafika walio bungeni
Watu wakazinduka, yaani wakashtuka wataongea nini
Watu na Bongo Flava kingine wanasema uzushi
Taarabu imeingia nuksi, Bolingo inafuka moshi
Sasa wahisani tapeli hutuboa wenye mistari
Kila mtu anakuja na uongo ili mradi tukubali
Na ma-producer wa sasa wanashtuka kwamba tunauza
Wanashtuka kwamba walicheza, Hip Hop ina fedha
Jay Moe mbakiaji sasa nahitaji umaskini u-bounce
Shori mzuri, gari, pamba, fedha kwenye bank account
Labda tatizo iwe kwa emcee asiye na elimu
Eti afanye nini? Mi nadhani bora akauze ndumu
[Hook – Professor Jay] x2
Hii ni tathmini kwa wote juu na chini
Yoh emcee zunguka nyuzi 360
Umeona nini? Mwana mpotevu rudi kundini
Fani ni uwanja mpana na jua lipo utosini
[Verse 3 – Professor Jay]
Yule yule ni Jay na Jay ni yule yule
Wanga wekeni kikao kisha mnifanye msukule
Domo langu ni hela linatoa ushauri wa bure
Ila ma-emcee wengi wa Bongo hampendi kwenda shule
Kumbuka hii ni rap ndani ya karne ya 21
Ni lazma uchemshe bongo kwenye mchanganuo wa hoja
Nafurahi kuona emcees ni wengi kama utitiri
Kinachoniudhi wengi wana-rap bila kutumia akili
Rap ya Bongo imegawanyika makundi mawili
Na kuna ma-emcee kamili na emcee waliobatili
Emcee mwenye hekima anafikiri kabla ya ku-rap
Na emcee mpumbavu ana-rap apate nyapu
Natumia lugha kali tafsiri unavyoweza
Napunguza tafsida maneno yanajieleza
Watu viwango vidogo wanaleweshwa na sifa
Ni lazma mjikongoje kwenye level za kimataifa
Wengi hampendi kuchambua temethali za semi
Na matokeo ndo vile ngoma zenu mwali hanemi
Watu wanavaba mic na ku-rap kama majuha tu
Katikati ya bahari mnapanda boti za mabua
Msilete utani, hii ni fani yenye ushindani
Jiulize waliovuma wangapi wamebaki gizani
Ninaowaudhi, hii naifanya makusudi
Ili mpate ghadhabu na kuongeza juhudi
[Hook – Professor Jay] x2
Hii ni tathmini kwa wote juu na chini
Yoh emcee zunguka nyuzi 360
Umeona nini? Mwana mpotevu rudi kundini
Fani ni uwanja mpana na jua lipo utosini

chemsha mongo lyrics by professor jay

[Hook]
Mwokozi nitoe roho niepuke hili balaa
Maisha nilichezea leo hii nalala njaa
Chemsha bongo kabla hujavagaa, ukashangaa
Chemsha bongo kabla hujavagaa, ukadua
[Verse 1]
Kwa kifupi nimekulia kwenye maisha ya kitajiri
Wazazi walinipenda walinipa lile na hili
Na tangu nikiwa mdogo nilionesha kwamba na
akili
Sio siri nilikimbia umande kusoma niliona sio
dili
Maisha yalikuwa matamu, nilisahau ya jehanam
Ilitakiwa uwe na hali flani upate yangu salamu
Washikaji niliwapita maskani kama vijisanamu
Wazee wenye busara walisema kijana hana
nidhamu
Hawakuumiza kichwa, niliamini hawatanilisha
Hawatanivisha, na hawajui utamu wa maisha
Mi ndo mimi mwendo mdundo, wengine niliona
uvundo
Niliamini naweza kula muwa pasipo kuvuta
fundo
Walisema mafumbo, fedha kwangu ni kama
nyundo
Na kila aliyenigasi sikusita kumjibu utumbo
Nilibadili mikoko mbali mbali ya kifahari
Nilikuwa napanga kreti za bia wapambe waoshee
gari
Mademu walijigonga, mashangingi walinipenda
Nilikuwa na toto mbili kila kiwanja nilichoenda
Niliitwa millionaire Bill Gates, mzee wa kuku
Wapambe walipepelea we we mambo ipo huku
Na kila aliyenigasi sikusita kumpatia buku
Aliyejifanya kiburi hakutafuna yangu ruzuku
Tulikuwa tukihama hama leo O’bay, kesho
Mikocheni
Nilikuwa nabadili baa leo Side Boy, kesho kwa
Macheni
Werevu walinishauri nilisema wanga niacheni
Na ka hamna shughuli kasukumeni mikokoteni
[Hook]
Mwokozi nitoe roho niepuke hili balaa
Maisha nilichezea leo hii nalala njaa
Chemsha bongo kabla hujavagaa, ukashangaa
Chemsha bongo kabla hujavagaa, ukadua
Mwokozi nitoe roho niepuke hili balaa
Maisha nilichezea leo hii nalala njaa
Chemsha bongo kabla hujavagaa, ukashangaa
Chemsha bongo kabla hujavagaa, ukadua
[Verse 2]
Kila club niliyoingia, wapambe walishangilia
Kwa kuwa walipata hakika ya kula kitimoto na
bia
Mademu waligombania, kila mmoja
kunikumbatia
Wengine walikuja kwa nyuma, “Jay
tunakuzimia”
Nilikuwa na desturi kila kiwanja nafunga baa
Niliposema wote kunyweni bure, hakuna
aliyeshangaa
Siku moja nilikuwa beach na demu mmoja
kipenda Zuwana
Asikwambie mtu jibaba nilikuwa na hela!
Nilikuwa nimepaki Mercedes Benz, convertible
eboh!
Ilikuwa nyeusi, rims za gold
Si ya hela kidogo
Wapambe walikuwa wamepamba Range Rover
nne nyekundu
NIlikuwa naongea kwa nyodo huku nikicheka
kizungu
Nilifanya vurugu ya mwaka na ushenzi
tulivyotaka
Maji tunatoa juu wangwana walibaki nyaka
nyaka
Tulivunja sheria za barabara na trafki alichekelea
Alijua akizuia msafara bosi wake atamfokea
Fedha iliongea, hakuna aliyenisogelea
Na kila aliyenigasi aliozea Segerea
Ila wazazi walinihusia kwamba urithi wangu ni
elimu
Niliamini unasoma upate fedha hivyo sikuona
muhimu
Kwa kuwa nilikuwa kiburi ndugu zangu
hawakunipenda
Mtukutu jeuri familia yangu ilinitenga
Nilianza kula mtaji nionekane bado natesa
Niliuza gari zangu tatu na nyumba nikabaki na
Chaser
Maisha yalianza ku-change madeni yakawa
mengi
Kuna wakati nilikimbia na kwenda kujificha
Zenji
Viwanja nilivyozoea hivi sasa nikawa siendi
Wale mademu na wapambe wote wakaanza
kuniona mshenzi
Wote walinikimbia na mbaya zaidi walinicheka
Walisema “Cheki Jay alosto ameshazeeka”
Nilianza kuweka bond mpaka vitu vyangu vya
ndani
Niliishi kama digidigi sikuonekana mtaani
Umaskini umepiga hodi kuishi sasa sikutamani
Sijui nilie na nani jamani nipo mashakani
[Hook]
Mwokozi nitoe roho niepuke hili balaa
Maisha nilichezea leo hii nalala njaa
Chemsha bongo kabla hujavagaa, ukashangaa
Chemsha bongo kabla hujavagaa, ukadua
Mwokozi nitoe roho niepuke hili balaa
Maisha nilichezea leo hii nalala njaa
Chemsha bongo kabla hujavagaa, ukashangaa
Chemsha bongo kabla hujavagaa, ukadua
[Verse 3]
Ilitokea ajali mbaya, wazazi wangu wote wakafa
Nikajua wataridhi mali kutokana na hayo maafa
Nikajipo moyo mi ni mzuka niliyefufuka
Ingawa nilikuwa na macho kumbe nilikuwa
nimepofuka
Vilianza tokea vizingiti na sielewi vilipoibuka
Watoto wa nje na mama wa kambo walipandisha
hulka
Wajomba na mashangazi wote wakawa
wamecharuka
Akili ilianza kuruka, harufu ya damu ilianza
kunuka
Waligombea mali nikaona ni heri kufa
Matajiri ombeni kwa Mungu kabla ya siku ya
kuanguka
Binadamu ni kama maua, kwani huchanua na
kunyauka
Na fedha ni kama shetani ukiwa nayo huwezi
tukuka
Dunia kizingiti, yataka mkono wa Mungu
kuvuka
Nenda kwa mapozi, mwenzio nalia
nimeshaumbuka
Hapa nilipo nanuka kikwapa, sijiwezi mchafu
kunuka
Mwili wangu ni kama kipande cha muhogo jinsi
nilivyopauka
Hutakiwi kucheka, walimwengu kweli najuta
Mbele ya Mungu na hii dunia naamini milango
itafunguka
Chini ya miguu, mwana mpotevu naanguka
Bible na Quran vinasema samehe anayejuta
Wananchi wenye ghadhabu bado wananipeleka
puta
Walitaka kunichoma moto, walishaniloeka
kwenye mafuta
Fanya hasara ya kunitafuta, kila saa na kila
nukta
Usitake yakukute ndugu yangu yalionikuta
Yoh..
[Hook]
Mwokozi nitoe roho niepuke hili balaa
Maisha nilichezea leo hii nalala njaa
Chemsha bongo kabla hujavagaa, ukashangaa
Chemsha bongo kabla hujavagaa, ukadua
Mwokozi nitoe roho niepuke hili balaa
Maisha nilichezea leo hii nalala njaa
Chemsha bongo kabla hujavagaa, ukashangaa
Chemsha bongo kabla hujavagaa, ukadua

Niamini lyrics by professor jay

[Hook – Professor Jay] x2
Niamini (sema)
Nataka uwe na mimi (mama)
Watu wenye fitina wanaleta majungu uachane na mimi (ye ye ye)
Hivi kwanini (sema)
Hutaki kuniamini (mama)
Nyoyo ziko pamoja mpaka siku ya kifo uanze we au mimi (ye ye ye)
[Verse 1 – Professor Jay]
Nakupenda sana ingiwa wanakuita demu wa uswazini
Penzi lako la kweli ndo kitu nachothamini
Kipepeo cha moyo we sema unachotaka
Jinsi unavyoenzi kipenzi sina mashaka
Tulipanda milima tukaja kwenye mabonde
Na sasa ni tambarare tufanye wanga wakonde
Kote tunakopita wamemwagia mbigiri
Njoo nikumbatie tufe tukiwa wawili
Hushangai, tukigombana tu wanafurahi
Na tukiwa pamoja wanashindwa kutusabahi
Walishakuja kwangu kunipa habari zako
Nikawatoa mbio kulinda heshima yako
Kwangu wamenishindwa wamegeuza kibao
Changanua mapema upime akili zao
Ni maisha yo Liz, twende tujikongoje
Maisha safari ndefu sijui mbele kukoje
Wanasema mi nakunywa wee, nalala kwenye baa
Wanasema mi ni bingwa la ngono kwenye mitaa
Wanasema mi nimeshawataka wamekataa
Kwako napiga goti yoh twende ki-superstar
[Hook – Professor Jay] x2
Niamini (sema)
Nataka uwe na mimi (mama)
Watu wenye fitina wanaleta majungu uachane na mimi (ye ye ye)
Hivi kwanini (sema)
Hutaki kuniamini (mama)
Nyoyo ziko pamoja mpaka siku ya kifo uanze we au mimi (ye ye ye)
[Verse 2]
Yoh, nikwamba
Mi nashukuru sana, umeniamini kwa sana
Hukufata maneno ya wanga waliochonga kwa sana
Miss Manana baab kubwa, hiyo ndo dhana
Wala hukunikana asante sana mi sitokukana
Tulifarakana tulikaa chini, tukapatana
Bila kugombana na ndio maana hatujatengana
Tukasamehana bila kutosana, endelea kukazana
Visa vizabina maji ya shingo sa chupi zinabana
Vichwa vinagongana wanaulizana, hatujaachana
Wanapigwa na bumbuwazi kuona bado tunakumbatiana
Tunashirikiana, na tunafanya vitu vya maana
Na haki ya Mungu mi nakuahidi mi ndo wa dhamana
Nakata mzizi wa fitina we ni wangu wa kuzikana
Mwingine hakuna, vita vya manyoya sasa hapana
Kwani maneno yalizidi hasa kwa wanga na mahasidi
Na wengine waliahidi lazma watumwagie acid
Eti hakomi kutupwa na napiga sana mchupa
Hautachukua round kwangu mi ntakutupa
Haukufanya pupa haukuogopa, haukunitupa
Ya Mungu mengi leo hii mambo ni super
Na yote aliyoahidi kwangu mi lazima kukupa
Usiwe na pupa, tulia, mi ndo simba
Unanipaga hamu, na hilo napenda ufahamu
Nakumbuka maneno yako matamu, mi nakupenda wewe
Unanipa kiwewe, ubavu wangu wa pili ni wewe
Napenda uelewa, niamini ni mimi na wewe
[Hook – Professor Jay] x2
Niamini (sema)
Nataka uwe na mimi (mama)
Watu wenye fitina wanaleta majungu uachane na mimi (ye ye ye)
Hivi kwanini (sema)
Hutaki kuniamini (mama)
Nyoyo ziko pamoja mpaka siku ya kifo uanze we au mimi (ye ye ye)
[Verse 3]
Amini amini, tuko pamoja safarini
Wala sigeuki, nipo pamoja na wenye chuki
Hivi ujabaini? Wanakudanganya maneno lukuki
Eti napenda chini, eti nakuhasi na hugutuki
Hivi inaingia akilini? Ni muda gani na ni lini!
Siku hiyo hatukuwa pamoja? Kama si huzushi ni nini?
Wanga wanajikongoja navyokupenda kwa ukalando
Mwana wametunga hoja, tutengane iwe furaha
Iwe tazamia vioja, usiwaamini hata mara moja
Wengi ni vizabi zabina, wapiga majungu na wafitina
Magwiji washirikina, pima vyema tena kwa kina
Tusije tukaachana, tutawapa msemo wageni iwe meno
Itakuwa haina maana, mara tu tumefarakana
Pia itakuwa aibu, tujaribu tu kuvumiliana
Mapenzi ni taratibu, mambo ya jana sio ya leo
Tusije tukaharibu, hebu sikia sogea karibu
Nani wa kunigiribu? Kwako sioni, sisikii
Ukiacha utaniadhibu, we nipe raha, nipe zabibu
Mpaka ntakapokufa, tushirikiane kuziba ufa
Wanga wasitufate, nafurahi unavyonipenda
Sinyo nasema asange, we nipe denda, nipe mate
Mama subiri fungate, mzizi wa fitina tena tukate
Wewe na mimi (mimi), niko radhi kula yamini
Wewe na mimi (mimi), mama Lily hebu niamini

Zani la mentali professor jay ft juma nature

[Verse 1 – Professor Jay]
Naamka asubuhi niko chwiri tena mapema
Nautoa mkeka sakafuni kisha naukunja vema
Nawaza nitakula nini mentali kisha naguna
Naanza kujikongoja kichwa chini mikono nyuma
Naelekea kilingeni nilikopaki mkokoteni
Nasaga na rumba kimshazali nyie acheni
Nawapa Hi machizi wananipa peace tunafurahi
Tunapiga stori nyingi wallahi bila maslah
Mara napata zali napeleka kago uswahili
Wananipa buku mbili danga chee nazisunda chini
Wakati natoka huku kijasho chembamba kikinitoka
Nikaona toto ya nguvu nikajikuta nimeropoka
“Dada habari samahani naomba niulize swali”
Akajibu “maskini koma tafadhali hii ngoma aghali”
“Ehee unajua dada–”
“We vipi hebu nipishe!”
“Dada mbona mkali?”
“Wee kinyago, kubali yaishe”
Nikasema inshallah sawa hiyo yote kwa sababu ya fukara
Nisije nikakubaka nitupwe selo nikawe kafara
Nikaachana nae sehemu za nyuma akizitingisha
Nilikula kwa macho hadhi yangu haikuridhisha
Nageuza mkokoteni nakuelekea maskani
Nikawapa stori machizi wakanicheka ikawa utani
Siku moja nililemaa maskani sikuwa na tenda
Na nilikuwa nikitafakari ni vipi siku itakwenda
Kumbe kuna gari ilikuja na kupaki karibu yangu
Sikuweza kuisikia labda sababu ya njaa yangu
Nilishtushwa ghafla na mlio mkali wa honi
Nilipatwa na mshtuko na hofu kubwa moyoni
Kuangalia pembeni ilikuwa imepaki Toyota Surf
Kulikuwa na sura ngeni ya malaika akaomba tafu
Nilisita kunyanyuka kwa sababu nilikuwa mchafu
Na alitoa elfu kumi na alikuwa akitaka dafu
Nilipokea hela alichotaka nilimletea, akakipokea
Tabasamu zito akanitolea nilimpa chenji
Ohh no keep change, una mawazo mengi itakufariji weekend”
Alikunywa maji ya dafu alitupa na kunikonyeza
Niliganda kama nyamafu nikahisi alinibeza
Alinipa busu la huba shavuni akanichombeza
“I love You” akawasha gari akateleza
[Chorus – Juma Nature]
Zali la mentali limetokea wakati mimi nnjaa
Nikapendwa na demu mkali
Na kuwaacha watu wote wakinishangaa, katika mitaa
[Verse 2 – Professor Jay]
Zilipita siku mbili nikiwaza kilichotokea
Nikawaza yule ni mtu au jini amenitokea
Potelea mbali uchawi hauendi kwa mentali
Narudi nanyonya napuliza mentali nakuwa shwari
Nabeba rumbesa nakatiza Samora Avenue
Mara kwa ghafla mbele yangu inapaki Toyota Mark II
Ohh napata ghadhabu mara nyingi sipendi dharau
Naifuata gari kuanza kupaka mara nahema juu juu
Aah ni yule mrembo!
“Maskini pole sana mzigo mbona mzito kweli utafika nao salama”
Natabasamu “Oh nimeshazoea mama
Na namshukuru Mwenyezi Mungu kwani hii ni kama karama”
Anakuwa mnyonge anang’ata kucha anantazama
Anaaza kulia anatoa lesso anainama
Namwambia, “bibie ni mara ya pili tunaonana
Na sidhani kama ni mbaya iwapo tukifahamiana”
“Naitwa Vicky na miaka 22
Ni mtoto wa kipekee kwenye familia ya kitajiri”
“Oh naitwa Jay ukiniita fukara haukosei
Na naishi kwa nguvu za macho siku zenyewe hazisogei”
Alishuka toka garini na kusema “Jay nakupenda”
Akaruka kwangu mdomoni na kuanza kupata denda
Nilichomoka kwake na kuanza kurudi nyuma
“Tafadhali mpenzi Jay jamani nionee huruma
Acha kubeba mizigo panda ndani kwa ile mchuna
Twende Mbezi Beach kwangu upepo unapovuma”
“Sikiliza Vicky napenda tuwe marafiki
Lakini hadhi yako hutakiwi kuwa na mtu wa dhiki
Hata wazazi wako naaamini hawataafiki
Tajiri na tajiri, maskini sithaminiki
Tafuta kibopa mwenzio ili usishushe hadhi yako
Mimi sistahili hata kuwa kijakazi wako”
“Tafadhali Jay usitamke maneno hayo
Naomba unielewe haya machache niyasemayo
Hadi huu wakati mimi nimekupenda kwa dhati
Ukikubali niwe wako nitajiita mwenye bahati”
“Nimeelewa Vicky naomba niwahishe mzigo
Tajiri ni mkorofi anansubiri Migomigo
Na kila nikichelewa mwenzako napata kipigo
Nasaga na rumba jua na mvua kwa mpigo”
Tuliongea mengi akanipa hela za matumizi
Sikuwahi hata kuziona nilikuwa kama chizi
Niliacha kubeba mizigo penzi letu likaota mizizi
Watu wa uswahili wakasema natumia kizizi
[Chorus – Juma Nature]
Zali la mentali limetokea wakati mimi n’njaa
Nikapendwa na demu mkali
Na kuwaacha watu wote wakinishangaa, katika mitaa
[Verse 2 – Professor Jay]
Baada ya miezi mitano Vick alipata ujauzito
Tulifurahi sana mambo yakawa mpwito mpwito
Suala la kwenda kwa wazazi wake halikuwa zito
Walifurahi sana kuniona tukafanya tambiko
Walisema Jay maisha ya Vicky yapo chini yako
Tumefurahi mmpendana kumlea ni jukumu lako
Ilipangwa mikakati kamambe ya kufunga ndoa
Watu hawakuamini ka mimi Vicky nitamuoa
Ilifika siku ya siku mentali Jay ndani ya jumba
Na Vicky ndani ya shela hakuna uchawi wala ndumba
Tulishikana mikono ni nderemo na vifijo
Tukafunga pingu za maisha kanisani bila ya fujo
Furaha isiyo kifani lilifanyika bonge la party
Watoto wa uswahili walibeba wali kwenye mashati (duh!)
Zawadi zilizagaa, zilikuwa nyingi tena kemkem
Baba mkwe alitupa Benz, kiwanda, nyumba na BM
Acha zawadi nyingi kutoka kila sehemu
Nilikumbuka nikacheka nilivyoteswa na wale mademu
Mambo swadakta nipo na Vicky ndio my wife
Kidume nang’aa wanajigonga shenzi type (shenzi type)
Nilipokuwa arosto mlinikwepa kama ukoma
Mambo juu ya mstari kunisalimu mnaona noma
Sahivi napeta, nabadili gari full kipupwe
Mlio nicheka wanataka ardhi ipasuke
Naelekea kilingeni kuwapa dili machizi wangu
Tena mara kwa mara siwezi kuwacha asili yangu
Vicky ni Jay, Jay ni Vicky mustarehe
Kutoka ndani ya dhiki sa kila siku sherehe
[Chorus – Juma Nature]
Zali la mentali limetokea wakati mimi nnjaa
Nikapendwa na demu mkali
Na kuwaacha watu wote wakinishangaa, katika mitaa

Kikao cha Dharura lyrics by professor Jay

[Verse 1]
Nawashukuru sana wananchi kwa kweza kunipa kura
Nashangaa nimeitwa ghafla kwenye kikao cha dharula
Kikao kinaashiria kina maswali juu yangu
Hii inatokana na ndiyo mzee na ahadi zangu..
Naona watu ni wengi wananchi walio na maana
Najaribu kutafakari ni nini kinawachanganya!!
Nipo tayari kujibu maswali yenu zamu kwa zamu
Watakao uliza maswali na ningependa niwafahamu
Naitwa sajent Byemero kwa niaba ya jeshi la polisi
Nilikuwa nauliza zile helikopta zetu vipi?
Nafikiria kwanza kuanzisha chuo cha marubani
Vinginevyo mtapata ajali nyingi sana angani.
Baskeli hamjui kuendesha helikopta mtaendeshaje
Kila mtu aendeshe yake huko angani itakuwaje?
Mheshimiwa sisi wakulima ulituahidi matrekta
Na siku zinayoyoma tu mbona haujayaleta ?
Wakulima mngeendelea tu kutumia jembe la mkono
Serikali haina hela bajeti imefika kikomo
Naona kilimo cha mkono kiniendelea vizuri
Jamani kazeni mikono endeleeni kukaza misuli
[Hook]
Wananchi tupo pamoja hapo. (siyo mzee!)
Watanzania tunaerewana kule, (siyo mzee!)
Washika dau na wapiga kura pale (siyo mzee!)
Eeehh.. (siyo mzee) eti? (siyo mzee!)
Wakulima tupo pamoja pale, (siyo mzee!)
Wanafunzi tunaelewana kule, (siyo mzee!)
Mabahamedi na mapolisi pale (siyo mzee!)
[Verse 2]
Mabaaamedi ondoeni hofu kilio chenu nimekisikia
Ma benzi yenu yapo bandarini tayari yameshawadia
Nimemchagua kiranja ili anipe idadi yenu
Niwape funguo zenu muondoke na magari yenu.
Ulituahidi utatujengea barabara tano tano juu na chini
Hizo zote hatutaki tunataka moja tu ardhini
Kila siku tunapita barabara zinakuwa mbaya
Umeyafumbia macho mheshimiwa huoni haya?
Barabara ya makwekwe nimesha imwaga kifusi
Baada ya wiki mbili itakuwa safi kama urusi
Makandarasi wanafanya kazi kutoka china na madagascar
Kuhusu vibarabara naomba muondoe shaka.
Eeh vipi mzee mabomba kutoa maji na maziwa nchi nzima ?
Jamani naomba muulize maswali ya utu uzima
Mabomba kutoa maji na maziwa haiwezekani
Mlinukuu vibaya nasisitiza haiwezekani
Mzee hali ni mbaya si tungegawana vya kwako?
Kwenye kampeni zako si ilikuwa moja ya ahadi zako ?
Eeehh? kugawana vya kwangu hilo swala litakuwa gumu
Familia itanitazama ebo? nina majukumu
Imeandikwa kila mtu atabeba msalaba wake
Kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake
Mbona mnaniuliza maswali mengi kunikomoa
Jamani watanzania tunajenga tunabomoa
[Hook]
Wananchi tupo pamoja hapo. (siyo mzee!)
Watanzania tunaerewana kule, (siyo mzee!)
Washika dau na wapiga kura pale (siyo mzee!)
Eeehh.. (siyo mzee) eti? (siyo mzee!)
Wakulima tupo pamoja pale, (siyo mzee!)
Wanafunzi tunaelewana kule, (siyo mzee!)
Mabahamedi na mapolisi pale (siyo mzee!)
[Verse 3]
Wafanyakazi wa serikalini sasa nyinyi magari ya nini?
Daladala chungu mzima mnaweza kuwahi kazini
Nasema mnapenda sana starehe kuliko kazi
Na hiyo ndio sababu mnaharibu hiki kizazi.
Wanafunzi niliwahidi mtafanyia practical mwezini
Kabla ya kupeleka mi nilifanya utafiti
Nimengundua huko mwezini kweli kuna baridi sana
Na pia kunavitisho kuwepo kambi za osama
Mkinichngua tena mtakwenda huko mapema
Nanita tekeleza kila neno ninalo sema
Sema nimesongwa na haka kamuda
Mkiniongezea muda kila kitu babu kubwa
Wengine kimya na maswali yamepungua
Yeyote mwenye swali ningependa kumtambua.
Naona mnanong’ona na wengi mmekunja sura
Hii inaonyesha mmeridhika kunipa kura
Nadhani ndugu zangu tuko pamoja (aah wapi!)
Jamani tupunguzeni jazba basi kidogo (hatutaki!)
Sasa watanzania mbona mnaazisha vurugu
Nadhani mmesahau watanzania wote ni ndugu
[Skit – Babu Ayoub]
Eeeh? jamani nasema hivi kikao kimeahirishwa
Jamani maafande, afande Miraji.. afande Mzafalu
Afande nani.. Gondwe njooni mtusaidie huku
[Hook] x2
Wananchi tupo pamoja hapo. (siyo mzee!)
Watanzania tunaerewana kule, (siyo mzee!)
Washika dau na wapiga kura pale (siyo mzee!)
Eeehh.. (siyo mzee) eti? (siyo mzee!)
Wakulima tupo pamoja pale, (siyo mzee!)
Wanafunzi tunaelewana kule, (siyo mzee!)
Mabahamedi na mapolisi pale (siyo mzee!)

Nikusaidiaje lyrics by professor jay ft ferooz

[Verse 1 – Professor Jay]
Umesahau ulipotoka, hujui unapokwenda
Ukapata kiburi kuona mi nakupenda
Nilikuthamini na letu penzi kulienzi
Na leo siamini kama umenisaliti mpenzi
Kumbuka nilikukuta kijijini sitimbi
Umebeba mahindi na furushi la magimbi
Nguvu ziliniishia mithili ya kufa maji
Nafsi nayo ikakidi kwamba mimi nakuhitaji
Kigoli mwenye umbo kama la mdori
Wala sikutaraji ungepiga nami stori
Nilifurahi kuweza kukufahamu
Na nikakuahidi subiri zangu salamu
Kwa kuwa nilikwenda tu kumtembelea bibi
Yote yaliyojiri tu kumweleza ilibidi
Wote walishangaa kusikia namtaka mchumba
Kwani vijana wengi wa mjini tuna kasumba
Wakaweka kikao ndiposa niweze kutoa posa
Niliapa kujua iwapo ningekukosa
Walinikabidhi nirudi nawe mjini
Na nikakusisitiza mjini kuwa makini
[Chorus – Ferooz]
Nafsi yangu nilikupa uitunze mpenzi
Anasa za jiji zikakuchanganya
Mapenzi ukasaliti na ukanikana
Ukaniacha dunia ikiniandama
Kuwa nawe haitawezekana mpenzi
Nshampata ambae tunapendana
Majeraha makubwa yajadui moyoni
Mi nimeshamuachia maulana
[Verse 2 – Professor Jay]
Alikuwa mzuri mithiri ya malaika
Alipotua mjini Zubeda ni patashika
Hakika alionekana alikuwa mgeni wa jiji
NIlipovua viatu nilivikuta ndani ya friji
Alifanya vibwenga washikaji wakanicheka
Hakutaka kitanda alilala kwenye mkeka
Alipokuwa akiona magari alikimbia
Akimuona mtu kwenye TV anamuamkia
Kila alichofanya alikuwa anakosea
Nilimvumilia kwa kuwa hajazoea
Hakai kwenye sofa alikuwa anakaa chini
Mafuta ya kupikia eti anayapaka mwilini
Namnunulia soda hataki anataka togwa
Nikimletea keki hataki anataka boga
Majirani walimpenda sababu ya uzuri wake
Nasikitika mashangingi wakawa rafiki zake
Akaanza kunywa pombe alipokwenda kusuka
Usiku anatoroka tena kwa kuruka ukuta
Nilipokuwa natoka, nae nyuma antoka
Nikimtuma kitu anadai eti amechoka
Nikienda kazini ndani analeta mabwana
Magari ya kifahari yakawa yanapishana
Hakika starehe za dunia zikamtenda
Na hatimaye hata nyumbani pia akatoweka
[Chorus – Ferooz]
Nafsi yangu nilikupa uitunze mpenzi
Anasa za jiji zikakuchanganya
Mapenzi ukasaliti na ukanikana
Ukaniacha dunia ikiniandama
Kuwa nawe haitawezekana mpenzi
Nshampata ambae tunapendana
Majeraha makubwa yajadui moyoni
Mi nimeshamuachia maulana
[Verse 3 – Professor Jay]
Nilipigwa na butwaa, mtaani walinishangaa
Nilikosa raha hata nafsi ilikata tamaa
Sikujua huyu binti ni mzima au amekufa
Ilibidi niombe watu msaada wa kumtafuta
Kumbe anaonekana viwanja vya kila aina
Leo yuko na mzungu na kesho yupo na mchina
Nilipata shahuku ya kutaka japo kumuona
Ingiwa niliamini moyoni ingenichoma
Kweli tulimtafuta kwenye kumbi tofauti
Ili nihakikishe kweli hajapatwa na mauti
Nikamkuta casino la wadachi na walatino
Akigonga mvinyo, wa hashipapi, hashipinyo
Pechiechipinyo na pamba za mandarino
Macho yalinitoka mithiri ya zingonginyo
Hakika alipendeza kwa staili alizocheza
Na kila aliyemtazama alitamani kumchombeza
Kwa pozi na dharau alijifanya amenisahau
Akaniona takataka mbele ya washikadau
Ilibidi niondoke machozi yakinilenga
Shetani kashanitega na tunda langu kamega
Akapata mimba aliyempa hakumtambua
Na wote aliowafata eti wakakana kumjua
Zubeda na mimba yake hakuwa na pakuishi
Hakujua ale nini na vipi apate ridhiki
Ghafla hifadhi yake ikawa ni stendi ya basi
Siku nyingine mvua ilimnyeshea kupita kiasi
Akarudi nyumbani eti arudiane nami
Kurudi kwao hataki, mi na familia ndani
[Chorus – Ferooz]
Nafsi yangu nilikupa uitunze mpenzi
Anasa za jiji zikakuchanganya
Mapenzi ukasaliti na ukanikana
Ukaniacha dunia ikiniandama
Kuwa nawe haitawezekana mpenzi
Nshampata ambae tunapendana
Majeraha makubwa yajadui moyoni
Mi nimeshamuachia maulana

kipi sijaskia lyrics by professor jay ft diamond platnumz

[Verse 1 – Professor Jay]
Niliacha kazi nifanye muziki wakatabiri nitalost
Wengine wakanishawishi tuloge kuondoa mikosi
Nakomaa na muziki ingawa jua la utosi
Naamini wote tunapita na kamwe maiti haijioshi
Jina langu lishatumika sana kutajirisha watu
Nyota ndogo alishasema kuna watu na viatu
Bunduki haiui watu ila watu ndio wanaua watu
Dunia kama jalala tazama kwa jicho la tatu
Ni saa mbaya watu wanahusda na roho mbaya
Tunawaita watakatifu kumbe ndio ma-vampire
Yalisemwa mengi demu wangu alivyotoroka
Ni fundisho tosha na changamoto kwa mwanachoka
Nimepita mengi mitihani ya kila namna
Ndio maana mi sishangai wakiniita mbeba lawama
Washkaji wengine fake kwenye deal hawakujui
Wanadhani kila jogoo akiwika ni asubuhi
Riziki hamuwezi iziba labda mtaichelewesha tuu
Mnakesha mnishushe Mwenyezi ananipaisha
Kote mlikobana kidume ndio natusua
Mnanijua, nakamua, roho za wanga zinaungua
Platnum!
[Chorus – Diamond Platnumz]
Unaehukumu ni wewe Mwenyezi Mungu naomba unilinde
Kwenye hii vita milele basi nishike mkono nishinde
Unaehukumu ni wewe Mwenyezi Mungu naomba unilinde
Kwenye hii vita milele mwanachoka daima Nishinde
[Verse 2 – Professor Jay]
Walishazusha nimekufa, eti nimepata ajali
Washindwe na walegee Mwenyezi niepushie mbali
Wakasema nina ukimwi kwa kuwa nilikonda ghafla
Wanataka kunizika mzima kabla sijafa
Waliosema nina ngoma wengine tushawafukia
Wanaoomba nife leo naamini watatangulia
Mama pumzika pema, daima tunakulilia
Na bado wanachonga sana, but man the king is here
Daima mtaji wangu ni nguvu zangu mwenyewe
Simwamini mtu kamwe najiamini mi mwenyewe
Hata nikinywa maji wanadai nakunywa pombe
Mi sijali, I knock them hard Mwanalizombe
Bado tu napambana kibarua kisiote nyasi
Daima sitawadhuru wale wote walioniasi
Nikikaa kimya msidhani sijasikia
Sio bahati sio ngekewa ni sauti iliyobarikiwa
Holla!
[Chorus – Diamond Platnumz]
Unaehukumu ni wewe Mwenyezi Mungu naomba unilinde
Kwenye hii vita milele basi nishike mkono nishinde
Unaehukumu ni wewe Mwenyezi Mungu naomba unilinde
Kwenye hii vita milele mwanachoka daima Nishinde
[Verse 3 – Professor Jay]
Mungu walaze pema waliosemwa wakajiua
Ingawa wote tunapita naamini Maisha ni hatua
Maneno ya watu sumu, yanaponya na yanaua
Please nipe ujasiri mpaka siku ukinichukua
Wape nguvu wale wote waliokata tamaa
Maneno yanaleta hila na mzozo kwenye mitaa
Wanahesabu mabaya tuu na mema hawayaoni
Wanakuchekea machoni, wanakuroga moyoni
Wanacheka chinichini wakati una msiba
Wa kwanza kukutangaza kwa watu ukiwa na shida
Wanatamani wapangue kila Mola alichopanga
Wanatangaza Amani huku wameficha mapanga
[Chorus – Diamond Platnumz]
Unaehukumu ni wewe Mwenyezi Mungu naomba unilinde
Kwenye hii vita milele basi nishike mkono nishinde
Unaehukumu ni wewe Mwenyezi Mungu naomba unilinde
Kwenye hii vita milele mwanachoka daima Nishinde