Wednesday, 20 July 2016

BARUA LYRICS BY BUSHOKE

[Chorus] x2
Leo nimepata barua kutoka kwa mpenzi wa zamani
Anasema eti ameli-miss penzi langu la thamani
Bushoke, nimepata barua toka kwa mpenzi
Yule yule, aloutesa moyo wangu
[Verse 1]
Ni mpenzi ambae tulipenda sana
Ila tulikuja tengana baada ye kwende Kenya kusoma
Nilitamani kwenda nae, ila uwezo mimi sina
Aliniahidi akirudi, nitafunga nae ndoa
Nilidhani ni kweli mamaa, kumbe alikuwa ananidanganya
Nilidhani ni kweli mamaa, kumbe alikuwa ananidanganya
Mimi oh, mimi
Miezi miwili tu kupita, akanijulisha kwa barua
Amepata bwana mwingine, na wanapendana sana
Miezi miwili tu kupita, akanijulisha kwa barua
Amepata bwana mwingine, wanataka funga ndoa
[Chorus]
Leo nimepata barua kutoka kwa mpenzi wa zamani
Anasema eti ameli-miss penzi langu la thamani
Bushoke, nimepata barua toka kwa mpenzi
Yule yule, aloutesa moyo wangu
[Verse 2]
Kama ilivo Mungu hamtupi mja wake, mama ah
Akanijalia nami nikapata bibi oh
Kama ilivo Mungu hamtupi mja wake, mama ah
Akanijalia nami nikapata mpenzi oh
Niliompenda, alienipenda
Niliemthamini, akanithamini
Mwenye kuninyunyiza marashi ya upendo oh
Na kunitoa shombo la uchumba hewa
Mwenye kuninyunyiza marashi ya upendo oh
Na kunitoa shombo la uchumba hewa
Sasa leo hii mamaa, leo hii mamaa
Nimepata barua toka kwa mpenzi wa zamani
Anasema ya kwamba anataka eti kuwa nami
Nitafanya nini mimi, nami na mpenzi sasa
Anasema eti Mungu anasamehe na mi nisamehe pia
Eti Mungu anasamehe, na mi nisamehe pia
Kumpenda bado nampenda, msema kweli mpenzi wa Mungu
Ila nachofikiria mimi ni mpenzi wangu wa sasa
Mimi oh… Bushoke
[Chorus] x2
Leo nimepata barua kutoka kwa mpenzi wa zamani
Anasema eti ameli-miss penzi langu la thamani
Bushoke, nimepata barua toka kwa mpenzi
Yule yule, aloutesa moyo wangu

No comments:

Post a Comment