Verse 1 [Kidum]
Ikiwa umeamua kunitoroka
Ikiwa unahisi hujiskii nami tena
Naona ni bora nilie leo, badala ya kesho
Kupenda, usipende Ni kama kujitia kitanzi
Nitachimba na sururu Kwa ardhi nikitafuta penzi lako
Ni heri nipigwe fimbo kwa mwili
Sababu ntajikuna ama ntajikanda na maji moto
Maumivu ya penzi, mtu hajikuni
Wala hajikandi na maji, na hakuna upasuaji
Chorus
Kama Kuna kosa nimewahi fanya (nielezee)
Kama Kuna jinsi tunaweza leta (mpaka niishi)
Na kama Kuna kitendo linaweza tendwa (nielezee)
Nitafanya (fanya) Nitatenda (tenda)
Nitafanya (fanya) Nitatenda (tenda)
Nitafanya (fanya) Nitatenda (tenda)
Nitafanya (fanya) Nitatenda (tenda)
Verse 2 [Lady Jay Dee]
Kweli hukumbuki ulioyafanya Ni kweli unakumbuka tulikotoka
Sisemi habari zozote za kusikia Bali kwa ushahidi niliouona
Msamaha mara ngapi Umeshaomba na bado
Chenye makosa mangapi Niliyoyafumbia macho
Mpaka leo nahisi kufika kikomo Maumivu yanazidi
Ndani ya moyo Sitaki kwenda mbali kwani uko moyoni
Nikusamehe mimi mara ngapi wee Nielezee mpenzi mara ngapi
Chorus
Unataka nikusamehe mara ngapi (usihesabu)
Ungependa nikuvumilie mara ngapi (hii ni ya mwisho)
Je wewe nikulilie mara ngapi (vumilia) Sitoweza (utaweza wee)
Nimechoka (usichoke) Nimeshindwa (usishindwe)
Naondoka (usiondoke) Sitoweza (utaweza yee)
Nimechoka Nimeshindwa (usishindwe)
Naondoka (usishindwe)
Verse 3
Ukihesabu mara ngapi umenisamehe Ni kama kuhesabu
Ni mara ngapi mtoto kaharibu nappy Usichoke
Usiondoke Usilie Niko hapa kukulinda
Chorus
Kama Kuna kosa nimewahi fanya (nielezee)
Kama Kuna jinsi tunaweza leta (mpaka niishi)
Na kam Kuna kitendo lingeweza tendwa (nielezee)
Nitafanya (fanya) Nitatenda (tenda)
Nitafanya (fanya) Nitatenda (tenda)
Nitafanya (fanya) Nitatenda (tenda)
Nitafanya (fanya) Nitatenda (tenda)
Unataka nikusamehe mara ngapi (usihesabu)
Ungependa nikuvumilie mara ngapi (hii ni ya mwisho)
Je wewe nikulilie mara ngapi (vumilia)
Sitoweza (utaweza wee) Nimechoka (usichoke)
Nimeshindwa (usishindwe) Naondoka (usiondoke)
Sitoweza (utaweza yee) Nimechoka
Nimeshindwa (usishindwe) Naondoka (usishindwe)
No comments:
Post a Comment