verse 1
Kama ni mapenzi Ya kuniudhi kila saa
Ya kunifanya mi kulia Na kama huridhiki
Na mbona hujasema Ili niweze rekebisha
Nifanye mambo shwari Nikiamini u kwangu
Na kukusifu kwa wazazi Hujali tenda hisia zangu
Sijui tunapokwenda Lakini najua tulipotoka
Kutoka sitoki nimetekwa nyara Kukuwacha siwezi kibarua ngumu
Nashindwa ni nini ntafanya uridhike Nimetekwa ndani
Mtandao wa mapenzi Basi nakuomba
Uniteke tu bila mateso
Chorus
Tazama, nimezama Ndani ya bahari, la penzi lako
Siwezi, kusonga mbele Kurudi nyuma, sijielewi
Haya mapenzi ya fujo hayafai Kama wanipenda, jaribu kunipa raha
Verse 2
Mi nashangaa, watu wakisema
Eti tunapendana, japo tunazozana
Ni vizuri mami, nyumba kuwa na siri
Lakini jaribu, tusuluhishe
Bila hivyo, itakuwa mchezo
Wa kuigiza, kwenye mambo bandia
Mimi sitaki, mambo ya kujifanya
Ati tunapendana, tena tunatesana
Nimejaribu sana kujitoa ndani
Kila nikipanga napangua mwenyewe
Natamani sana ungeelewa hivyo
Mimi mateka Mimi pumbavu
Wa penzi lako Nieleze ni lini ntakuwa huru
Chorus
Tazama, nimezama
Ndani ya bahari, la penzi lako
Siwezi, kusonga mbele Kurudi nyuma, sijielewi
Haya mapenzi ya fujo hayafai
Kama wanipenda, jaribu kunipa raha
Verse 3
Jaribu baby
Mambo ya kunifanya kumbafu haifai
Mambo yo yo yo yo yo
Haifai
Jaribu baby, tusuluhishe
Nimejaribu sana kujitoa ndani
Kila nikipanga napangua mwenyewe
Natamani sana ungeelewa hivyo
Mimi mateka, mahabusu
Wa penzi lako
Nieleze ni lini ntakuwa huru
Chorus
Tazama, nimezama
Ndani ya bahari, la penzi lako
Siwezi, kusonga mbele
Kurudi nyuma, sijielewi
Haya mapenzi ya fujo hayafai
Kama unanipenda, jaribu kunipa raha
No comments:
Post a Comment