Wednesday, 13 July 2016

MULIKA MWIZI LYRICS BY KIDUM FT SANAIPEI


Verse 1

Ukiona mwanaume kwa hali ya kulia, jua yakwamba ameguswa pahali

Sio rahisi, si kawaida kushuhudia mwanaume akitoa machozi

Hapo zamani nilidhani mwanaume akipoteza kazi ndio uchungu, ndio unyonge 

Kumbe mapenzi ndio sumu kali, inayofanya mwanaume kulia

Kama mtoto mtoto, kama kidogoyo

Hapembelezwi, hanyamazishwi, machozi yake inatoka ikienda tumboni

Hapembelezwi, hanyamazishwi, machozi yake inatoka ikienda tumboni



Chorus

Mulika mwizi, mulika na tochi, mulika (mulika mwizi)

Mulika mwizi, kama kuna giza mulika

Nimulikie mwizi, nasumbuka, nataka kujua nani mwizi wa mapenzi

Barua pepe kwa simu ya rununu, ujumbe mfupi unafutwa na sekundi tatu (sekundi tatu)

Nilimpenda baibe wangu, nikampea roho yangu, amechukuliwa, amenyakuliwa

Jamaa fulani hapa mtaani, mwenye magari, na mapesa, amechukua baibe 

Ikanifanya crazy,sipembelezwi, sinyamazishwi
Machozi yangu yanatoka yakienda tumboni

Msiomboleze, mnamujua huyu jamaa, kajifanya bubu, wengine vipofo




Chorus

Mulika mwizi, nimulikie mwizi

Nimulikie mwizi, nasumbuka, nataka kujua nani mwizi wa mapenzi

Nani mwizi wa mapenzi



Verse 3

[Sanaipei]

Ukiona baibe wako anaingia bafu na simu mkononi, huyo ni mwizi (mulika mwizi)

Uniona mzee wako anazima simu kila mara akiwa kwa nyumba, mulika mwizi (mulika mwizi)
 Oh-o-o-o oh oh  oh-o-o-o
Oh-o-o-o –o-o


Nimulikie mwizi jameni, (mulika mwizi)

Mulika mwizi, nionyeshe, niambie ni wapi

Nimulikie mwizi, mwizi wa mapenzi, mwizi wa mapenzi (mulika mwizi)

Nani mwizi wa mapenzi

Nani mwizi wa mapenzi (mulika mwizi)

Wani ua, wani umiza (oh –o-o-o-o)

Mulika na tochi, natazama mbele si nyuma

Mulika mwizi, kila mtu mwizi wa mapenzi, kila mtu mwizi wa mapenzi


Pia mimi mwizi wa mapenzi

No comments:

Post a Comment