Monday 25 July 2016

Dunia Mapito lyrics by Matonya

[Verse 1]
Aah dunia
Bado nikiza, bado nikiza
Na marashi ya dunia siyasikii
Najihisi nipo kuzimu naishangaa sayari hii
Iliyojawa wanasiasa, michezo na wasanii
Najiuliza wamekuja huku kutalii
Au wameshahamia dunia ndo haijirudii?
Mara nasikia swali kama la nguvu za hoja
Dandu ananiuliza ‘albamu zinajikongoja?
Vipi mmegonga copy chini ya milioni moja?’
Jibu zinalipa sio moja kwa moja
Steve 2K anauliza ‘bifu zinaendeleaje?
Nimesha msamehe Casto ameshatoka Segerea?’
Namjibu bifu lipo na vita vinanyongea
Casto bado anaoza, tuanzeni kumuombea
Complex naye anauliza ’albamu ile ya wagosi
Walishagonga kopi ngapi hadi sasa kwa wadosi?
Namjibu tangu ufe mambo yote ni mikosi
Makundi yanavunjika duniani tunakumiss
[Chorus]
Yee iye iye eh
Dunia mapito jamaa
Tuwaombeeni waliokufa wende salama
Mi nawe tupo hatujui siku yetu lini
Kinachotakiwa tuishi kwa amani duniani (mi na wewe)
Yee iye iye eh
Dunia mapito jamaa
Tuwaombeeni waliokufa wende salama
Mi nawe tupo hatujui siku yetu lini
Kinachotakiwa tuishi kwa amani duniani
[Verse 2]
Kulia nafuta chozi, kushoto lanidondoka
Nakosa raha TX Moshi nikimkumbuka
Muone ananiuliza ‘muziki wa dansi ndio ushashuka?’
Jibu bado upo, ila naamini pengo lako halitozibika
Mara kwambali nasikia sauti ya gitaa
Sauti ya gitaa inapigwa huku inaniita
Kumbe mzee wakale, hayati Bob Marley
Ananiuliza ‘mziki wa Reggae unaenda vipi?’
Reggae bado ipo
Ziggy na Damian na Jissy wanagonga copy
Marijani, ananiuliza ‘muziki wangu unaimbwa sana duniani
Vipi familia yangu inafaidika kitu gani?’
Jibu mimi sina labda mwanao Marijani
Kiza ni kinene sioni pa kupapasa
Mara kwa mbali nawaona wanasiasa
Machozi yananitoka, chini nadondoka
Namuona Karume na Nyerere Julius
Wananiuliza ‘muungano je una nafasi?’
Nawajibu msiwe na wasi
Sasa ari mpya, nguvu pia na kasi
Ulimwengu mmeuacha dunia ndio inawamiss
[Chorus]
Yee iye iye eh
Dunia mapito jamaa
Tuwaombeeni waliokufa wende salama
Mi nawe tupo hatujui siku yetu lini
Kinachotakiwa tuishi kwa amani duniani
Yee iye iye eh
Dunia mapito jamaa
Tuwaombeeni waliokufa wende salama
Mi nawe tupo hatujui siku yetu lini
Kinachotakiwa tuishi kwa amani duniani

No comments:

Post a Comment