Sunday, 3 July 2016

BARUA YAKO NIMEKWISHA IPATA LYRICS BY LES WANYIKA


Barua yako nimekwisha ipata sheri,
Nia yako tupendane wawili oo
Sikatai lakini kitu kimoja
Naogopa ee naogopa

Wanaokupenda watanipa taabu

Mimi masikini ee naogopa
Hali yangu ya unyonge sijiwezi oo ah mama
Elewa wazi kama tutapendana oo
Mabaya mengi yatanifuata fuata
Na mimi wenzio kamwe sijivuni oo
Nakuomba ee ufikiri oo ah mama..
Ukweli nakupenda lakini naogopa

Kwani kukabili wale wako wanaokupenda
Kukopa harusi kulipa matanga

Kupendana raha takapotupata balaa tuepuke mama

1 comment: